UFUGAJI WA KUKU

Tiba na chanjo dhidi ya magonjwa ya kuku.
Afya ya kuku huweza kuathiriwa na magonjwa ya aina nyingi, wadudu tofauti na lishe duni ambavyo husababisha hasara kwa mfugaji yasipodhibitiwa au kutibiwa mapema. Hasara hizo ni pamoja na gharama za matibabu, kushuka kwa utagaji mayai, kudumaa na hata vifo.
Dalili za kuku Mgonjwa;
Dalili za ujumla za kuku mgonjwa ni kama zifuatazo:-
• Kuzubaa
• Kupoteza hamu ya kula
• Kujitenga na wenzake katika kundi
• Kujikunyata
• Kupunguza au kusimama kutaga
Kumbuka: Ukiona dalili moja au zaidi ya hizi muone mtaalam wa mifugo aliye karibu.
Magonjwa ya kuku;
Vyanzo vya magonjwa ni virusi, bakteria, protozoa, minyoo, wadudu wa aina mbali mbali na upungufu wa virutubisho
kwenye chakula cha kuku na uchafu.
Magonjwa yanayosababishwa na virusi;
Kwa kawaida, magonjwa yanayosababishwa na virusi hayatibiki. Hivyo njia pekee yakukabiliana nayo ni kwa kuchanja ili kuyadhibiti kabla hayajatokea.
1;MDONDO
Ugonjwa unaosumbua sana wafugaji wa kuku ni Mdondo na wengine huuita Kideri (newcastle disease). Chanzo cha ugonjwa huu ni virusi. Ni ugonjwa unaoathiri kuku wa rika zote na mara nyingi humaliza kuku wengi au wote vijijini.
DALILI ZA MDONDO ni:
• Kuku hukohoa
• Kuhema kwa shida
• Hushusha mbawa
• Kupoteza hamu ya kula, kuzubaa, kusinzia
• Manyoya kuvurugika
• Kuharisha kijani
• Kutokwa ute mdomoni na puani
• Kizunguzungu, shingo kujikunja, kurudi kinyumenyume, kupooza mabawa, kuanguka chali, kupoteza fahamu na hatimaye kufa.
• Kuku wengi kwenye kundi hufa katika kipindi kifupi kwa kufikia asilimia 90 hadi 100.
UENEZAJI WA UGONJWA huu ni kwa njia zifuatazo:
• Kinyesi cha kuku anayeumwa kikikanyagwa na miguu, magari, baiskeli na kuwafikia kuku nwengine.
• Kwa njia ya hewa (kuvuta hewa yenye virusi ) au upepo waweza kusafirisha virusi.
• Mabaki ya kuku anayeumwa kama utumbo, manyoya n.k. visipozikwa vitaeneza ugonjwa kwa kuku wazima kula mabaki hayo au wanyama watakaokula mabaki hayo huweza kuyasambaza na kueneza ugonjwa.
KUDHIBITI MDONDO
Kuchanja
Kwanza kabisa ni chanjo ya Mdondo.
Zipo aina tofauti za chanjo ya Mdondo. Lakini chanjo iliyo rahisi kutumiwa vijijini inaitwa I – 2 Thermostable. Chanjo hii tofauti na chanjo nyingine nyingi inao uwezo wa kustahimili joto.
Hutolewa kwa njia ya kuku kudondoshewa tone moja la dawa katika jicho moja tu. Hii ni dozi kamili kwa kuku wa umri wowote.
Baadhi ya dalili za ugonjwa wa Mdondo
Kupambana na magonjwa ya kuku: Jinsi ya kutibu na kuchanja
Dawa hii upatikana kwenye maduka ya madawa ya mifugo au ofisi za serikali za mifugo.
Utaratibu wa kuchanja kwa dawa ya I – 2 Thermostable
• Mdondo hauna tiba kwa hiyo unakingwa kwa chanjo
Kuku wachanjwe mara baada ya kutotolewa bila kusubiri mzunguko au ratiba ya chanjo inayofuata katika eneo husika.
• Kuku wachanjwe kila baada ya miezi mitatu bila kukosa. Kama unayo kalenda weka alama kwenye tarehe za kuchanja ili uweze kufanya maandalizi mapema ya upatikanaji
wa dawa.
• Kuku wachanjwe angalau mwezi mmoja kabla ya mlipuko wa ugonjwa . Kwa kawaida wafugaji wanafahamu miezi ya mlipuko ya ugonjwa huu katika maeneo yao.
• Angalia sana uchanje kuku ambao hawajaambukizwa. Kuku akiishaugua chanjo haitasaidia bali itaongeza kasi ya ugonjwa.
• Japo chanjo ya I-2 Thermostable, ni muhimu ihifadhiwe sehemu kavu na yenye ubaridi wa kawaida isipate joto, la sivyo itaharibika na haitafaa tena kwa chanjo.
2.NDUI YA KUKU (FOWLPOX)
DALILI ZA UGONJWA;
- Vipele vya mviringo ambavyo huweza kuungana na kusababisha vidonda kwenye upanga, masikio na miguu hususan sehemu zisizo na manyonya.
- Utando mweupe mdomoni.
- Vifo hutokea kwenye vifaranga.
KINGA/TIBA
-Hakuna tiba
Kinga:
- Kuku wachanjwe dhidi ya ugonjwa wakiwa na umri wa miezi 2 au kulingana na maelekezo ya mtengenezaji wa chanjo.
- Kuku wakiugua wapewe (multivitamini) vitamin na antiobitic kama OTC 20% kutibu vidonda.
- Banda liwe safi wakati wote na hasa kudhibiti unyevu.
- Kutenga kuku wagonjwa ili wasiambukize wengine.
3. GUMBURO
- Ugonjwa huwapata vifaranga wenye umri kati ya wiki 3 hadi 8.
- Huambukiza idadi kubwa ya kuku na kusababisha vifo kwa asilimia 20 hadi 50.
- Kuku kuharisha kinyesi cha majimaji, hushindwa kusimama,
hutetemeka na hatimaye kufa.
KINGA/TIBA
Hakuna tiba
Kinga:
- Chanja vifaranga wakiwa na umri wa siku na urudie kuchanja baada ya siku 21.
- Kutenga kuku wagonjwa ili wasiwambukize wengine.
- Kuku wapewe antibiotic na vitamin ili kutibu magonjwa nyemelezi
4.MAFUA MAKLI YA NDEGE (Avian influenza)
DALILI
- Kupumua kwa shida.
- Kukohoa na kupiga chafya.
- Sehemu za kikole (kidevu na kishungi)) hubadilika na kuwa na rangi ya zambarau.
- Kutokwa na machozi,
- Kuku kupinda shingo na kuanza kuzunguka.
- Kuvimba kichwa
- Kuharisha kinyesi chenye maji maji, rangi ya kijani na
baadaye kinyesi cheupe.
KINGA/TIBA
- Ukiona dalili hizo toa taarifa kwa Daktari/Mtalaam wa Mifugo aliye karibu nawe.
- Ugonjwa huu hauna tiba.
5. HOMA YA MATUMBO(Fowl typhoid)
- Ugonjwa huu unaweza kurithiwa kupitia kwenye mayai au kuambukizwa kutokana na kuku wagonjwa, kinyesi, kudonoana na mazingira machafu.
- Kuku huharisha mharo wa njano vilemba na upanga hupauka kutokana na upungufu wa damu,
- Manyoya husimama.
- Vifo huweza kufikia asilimia 50.
- Kuzubaa, kuvimba viungo vya miguu, kuchechemea,
- Hukosa hamu ya kula.
- Kuku wanaotaga hupunguza utagaji, hutaga mayai yenye ganda laini.
- Kuku wanaopona huendelea, kusambaza vimelea vinavyosababisha ugonjwa.
KINGA/TIBA
- Kuzika au kuchoma moto mizoga na masalia ya kuku waliokufa kwa ugonjwa huo.
- Usafi wa banda na mazingira yake.
- Ondoa kuku wenye ugonjwa na usitumie mayai yenye ugonjwa kuangua vifaranga.
- Tibu kwa kutumia dawa zinazoshauriwa na wataalamu OTC 20%
powder
- Vile vile vitunguu swaumu hutibu. Chukua robo kilo ya vitunguu
swaumu, toa maganda. Kisha twanga, changanyana maji kiasi cha lita moja, chuja na kuwapa maji yake kwa muda wa juma moja.
ITAENDELEA NA MAGONJWA MENGINE; KWA MAWASILIANO /USHAURI/MAONI/ MAREKEBISHO NI TEXT/WHATSAPP NAMBA 0769189448.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU NA KU SHARE POST HII ILI KUSAIDIA WENGI!
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment