YANGA YAENDELEZA UTEJA KWA GOR MAHIA

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga leo imeshindwa kufuta uteja wake wa mara kwa mara kwa mabingwa mara tano wa Kombe la Klabu bingwa Afrika mashariki na kati baada ya kupigwa bao mbili kwa moja. licha ya Yanga kuwa ya kwanza kuliona lango la Gor Mahia lakini iljikuta ikitoka uwanjani kichwa chini baada ya Gor Mahia Kusawazisha bao dakika ya 18 na kuongeza bao la pili na la ushindi dakika ya kwanza ya kipindi cha pili kupitia kwa Michael Olunga. Yanga ilipata bao baada beki wa Gor mahia kujifunga kufuatia krosi maridhawa iliyochongwa na Donald Ngoma kutoka winga ya kushoto. baada ya bao hilo yanga walitawala mchezo huku Gor Mahia wakionekana kupoteana uwanjani. lakini dakika ya 18 Gor Mahia ilisawazisha bao kwa mpira wa faulu uliopigwa na Dirkir Glay wa faulu uliopigwa na . ushindi wa leo wa Gor Mahia unaendeleza historia ya vipigo kwa Yanga kutoka kwa mabingwa hao wa ligi kuu ya Kenya. katika mchezo huu klabu ya Yanga ilikosa penati ilyopigwa na nahodha wake Nadir Horoub "Cannavaro" dakika ya 73 huku mshambuliaji wa timu hiyo Donald Ngoma akitolewa kwa kadi Nyekundu dakika ya 25.
kikosi cha yanga katika mechi ya leo kiliundwa na Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Joseph Zuttah dk75, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Simon Msuva/Kpah Sherman dk69, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Salum Telela dk84. 
huku kile cha Gor Mahia kikiwa na Boniface Olouch, Mussa Mohammed, Sibomana Abouba, Harun Shakava, Kari Nzigiyimana, Dirkir Glay, Khalid Aucho/Erick Ochieng dk89, Godfrey Walusimbi/Ronald Omino dk86, Innocent Wafula/Enock Agwanda dk86, Medie Kagere na Michael Olunga.
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :