MGOMBEA LUDEWA; HAKUKUWA NA UCHAGUZI

Uchaguzi wa Ludewa ilikuwa kiinimacho cha demokrasia. Tulipewa barua na msimamizi wa uchaguzi kuwa mawakala wataapishwa tarehe 16/12/2015. Lakini tulipowapeleka watu wa kuapishwa, katika kata 16 mawakala walikuwa tayari wameapishwa, na tuliowapeleka tarehe 16 waliokubaliwa kuapishwa ni katika kata 2 tu, wengine wote walikataliwa kwa maelezo kuwa uapishaji ulikwishafanywa.
Kata ya Mundindi, mawakala wetu waliokuwa ndani ya ofisi ya mtendaji wa kata wakiapa, walifukuzwa na Mkuu wa Wilaya aliyeambatana na polisi kwa maelezo kuwa siyo wakazi wa kata ya Mundindi.
Iwela, tarehe 18, siku mbili kabla ya uchaguzi, mtendaji wa kata alikutwa na mmoja wa mawala wa CCM wakijaza kura kwenye fomu za matokeo. Walipoulizwa walikuwa wakitetemeka na kudai kuwa zilikuwa ni fomu za mfano.
Mkuu wa wilaya katika maeneo mbalimbali alipiga marufuku wageni kuingia Wilaya ya Ludewa mpaka wapate kibali kutoka kwake, akisema kuwa ana taarifa kuwa CHADEMA imeingiza magaidi. Kata ya Mkomang'ombe mawakala wetu waliotoka Ludewa mjini walikamatwa na mtendaji wa kata, walipigwa na kuwekwa kwenye cell ya kata.
Kuna maeneo ambayo mawakala wetu walitutumia matokeo ya awali ambayo baadaye yalikuja kuonekana ni tofauti na waliyoyasaini kwenye fomu za matokeo, huku namba zikiwa zimebadilishwa, tulizoambiwa awali ni za CHADEMA, zimekuwa za CCM, na za CCM zimekuwa za CHADEMA. Je, tofauti hiyo ilisababishwa na uelewa mdogo wa mawakala au walikula njama baada ya kumaliza mchakato wa uchaguzi?
Mkuu wa wilaya akitumia rasilimali zote za serikali, muda wote alisimama jukwaani kumpigia kampeni Ngalawa akiwatisha watu endapo kama hawatamchagua!
Japo sitarajii kugombea, nawasiliana na wanasheria ili kuona kama tuna sababu za msingi za kupinga matokeo. Tukiacha uhuni huu uendelee kwenye uchaguzi, nchi hii haitapiga hatua katika demokrasia. Japo inagharimu rasilimali muda na fedha, ni lazima tupiganie ili uhuni kwenye uchaguzi tuendelee kuupunguza au kuufuta kabisa kwa manufaa ya watu wote. By msambicha, mgombea ludewa
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment