NAIBU WAZIRI: Mheshimiwa umepata tarifa za mkutano wa mawaziri utakaofanyika Ujerumani wiki hii ?
WAZIRI: Ndio nimesikia, inatakiwa kwenda maana nimhimu sana.
NAIBU WAZIRI: Unaenda wewe au niende mimi ?
WAZIRI: Nitaenda mimi maana nina mambo mengi sana ya kujadiliana na
wenzetu wa nchi mbalimbali ili tupate suluhu la matatizo ya wizara yetu.
NAIBU WAZIRI: Sawa mkuu, basi jiandae uende naamini utarudi na mambo mengi ya msingi.
WAZIRI: Sawa, ngoja nikamuage mheshimiwa Rais.
>>>>Waziri anaingia kwenye gari lake kuelekea magogoni kwenye Ikulu ya nchi kwa mazunguzo na mheshimiwa Rais.
RAIS: OOOh karibu mheshimiwa .
WAZIRI: Asante sana mkuu.
RAIS: Kumbuka lakini nchi haina hela hivyo hata maji tu leo hakuna, au umeshakula kwako ?
WAZIRI: Usijali mkuu nimekula tayari.
kisha anacheka kidogo.
RAIS: Umekula kwako au hela za wizarani ??
WAZIRI: Nimekula kwa ndugu yangu mmoja maana hata familia yangu pia haina hela kama serikali.
Rais anacheka kidogo, kisha anakaa kimya kuashiria waziri anaweza kuendelea na maongezi yaliyompeleka Ikulu.
WAZIRI: Mkuu, kuna mkutano mkubwa unafanyika Ujerumani wiki hii unahusu
wizara yangu na ni mhimu sana kuhudhuria, ningependa kukuaga niende kwa
maslahi ya taifa.
>>>Rais anaonekana kuchukia kidogo kisha anaongea.
RAIS: Nilishasemaje kuhusu safari za nje ? au nikufute kazi mara moja ?
>>>>Waziri inamchukua muda kueleza umhimu wa ule mkutano
mpaka Rais anamwelewa, kisha Rais akainuka na kufungua kabati akachukua
simu ya kiganjani na kumpatia waziri.
RAIS: Shika hii simu uunge kifurushi cha international (cha kimataifa) umalizane nao hapa hapa.
>>>>Waziri akiwa bado anashangaa maamzi yale anakumbana na swali toka kwa mheshimiwa Rais.
RAIS: Au huna namba ya waziri wa nchi yeyote aliyehudhuria umwambie
arecord clips akutumie kwa whatsap nawe umchangie kwa whatsaap ?
>>>>Waziri inambidi awe mpole anasema sina.
Kisha Rais anafungua komputa na kumwambia waziri atumie mtandao wa skype kuwasiliana na mawaziri walioko ujerumani.
>>>>Waziri anajifanya kuchunguza simu yake kisha anaongea.
WAZIRI: Mkuu nimepata taarifa mpya wanasema mawaziri wote wahudhuri isipokuwa wa Tanzania.
RAIS: Hayo ndio mambo ya msingi, hebu fikiria mkiondoka ziara za kustukiza atafanya nani kwenye wizara yenu ?
>>>>Waziri anaamua kuaga na kuondoka kurudi ofisini kwake na kumkuta naibu waziri wake.
WAZIRI: Mkuu anasema tuunge kifurushi cha international tumalizane na walioko Ujerumani kwa simu !
NAIBU WAZIRI: Najua mkuu yeye hana udhoefu na masuala ya international affairs ndio maana anaogopa sana nje.
>>>>Kisha naibu waziri anajishtukia anauliza "Au unanirecord mheshimiwa ?"
WAZIRI: Siwezi kufanya utoto huo.
>>>>Naibu waziri anaendelea.
NAIBU WAZIRI: Unajua nje alienda mara moja tu mwaka 2003 alipodondoka
Bungeni akapelekwa India, tatizo lake la moyo huwa linamsumbua hata
akikaa kwenye ndege muda wa masaa mawili tu.
WAZIRI: Ngoja tusijihangaishe tule mshahara tu na kuzunguka na waandishi wa habari kila sehemu tumlidhishe .
Home
/
HABARI
/
SIASA
/
VICHEKESHO
/
SIJUI KAMA HAYA YANATOKEA BAAADA YA MHESHIMIWA RAIS KUKATAZA BAADHI YA SAFARI ZA MAWAZIRI NJE YA NCHI
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment