FAHAMU HAYA KUHUSU MATAIRI KWA WENYE MAGARI;


Matairi ya gari muda wake rasmi wa matumizi ni miaka minne (4) tu toka yatengenezwe (sio toka uyafunge kwenye gari yako).
Ikishapita miaka minne toka tairi litengenezwe linaweza kupasuka wakati wowote. Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (*2603*) kuna kuwa na alama ya nyota mwanzo na mwisho wa hizo namba nne.
Namba mbili za kwanza zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipo tengenezwa. kwa mfano *2603* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 2003 au *2699* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 1999.
KAGUA MATAIRI YAKO USITUMIE TAIRI LILILO PITA ZAIDI YA MIAKA MINNE KWANI LINAWEZA PASUKA WAKATI WOWOTE.

Pia kila tairi limeandikwa uwezo wa spidi yake ukikimbiza zaidi ya uwezo wake itapasuka na hizo spidi zimeandikwa kwa herufi kama ifuatavyo
CODE SPIDI
F=============80
G=============90
J==============100
K==============110
L==============120
M==============130
N==============140
P==============150
Q==============160
R==============170
S==============180
T==============190
H==============200
Huandikwa hivi
280/R/70/13/150/S
Hapo herufi S inawakilisha spidi, 180
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment