Dr slaa akanusha taarifa za upotoshaji zinazotolewa na viongozi wa chadema kumhusu yeye

Dr Slaa amesema hivi  katika ukurasa wake wa jamiiforum
"Siasa ya unafiki sipendi. Nimenyamaza lakini naona mnazidi kunichokoza. Ni afadhali mngelikaa kimya kama nilivyonyamaza mimi. Uwongo wowote na upotoshwaji wowote sitauvumilia. Nitaukanusha hapo hapo. Hata kama una lengo lako ambalo silifahamu naomba sana usitumie jina langu. Nimefundishwa uwongo ni dhambi siko tayari kushiriki dhambi hiyo.



sina kikao chochote cha Secretariat sina mpango wowote ninaopanga kuwasilisha popote. Naomba watanzania wapuuze propaganda zote zinazofanyika kwa jina langu.


Ningehitaji kutuma taarifa yoyote kwa umma ningeliita Press Conference Mwenyewe au ningelitumia utaratibu wowote uliouliozoeleka.


Naomba kutoa onyo kwa mtu yeyote awaye, matumizi ya jina la Dr Slaa yakome."


taarifa hii inafuatia taarifa zilizosambazwa na mmoja wa wanachadema aitwaye Yericko Nyerere aliyeandika hivi
 Jioni ya leo Dr. Slaa katibu mkuu wa CHADEMA atawasilisha mpango mkakati wa ushindi mbele ya sekretariet tayari kuelekea cc kesho.

Hatua hiyo inafuatia jopo la wataalamu nane likiongozwa na Dr Slaa kujichimbia kwa wiki nzima kuhariri na kuchakata taarifa mbalimbali za umoja wa vikosi kazi vya vyama vinavyounda UKAWA,

Japo maneno na uzushi mwingi umezagaa mitaani lakini Dr hayumbishwi na hilo, mida ya usiku wa leo atawasilisha ripoti hiyo katika vikao vinavyofanyika kwa siri kubwa ili kuepuka maadui ambao kwasasa tunapigana vita nao usiku na mchana.

Kesho ndio rasmi Dr. Slaa atawasilisha mbele ya cc mipango mkakati hiyo ikiwemo Ilani nk.

Pipoooooooz!!!!"

 
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment