Awali mgombea ubunge huyo ndugu Cuthbert Ngwata pamoja na dereva wake walikimbiziwa katika hospitali ya Nyasa kwa matibabu lakini kutokana na hali zao kuwa mbaya sana wamehamishiwa kwenye hospitali ya Litembo kwa matibabu zaidi.
Hili ni tukio la pili kuwapata wagombea Ubunge wa Chadema katika kipindi kisichopungua wiki tatu. Ikumbukwe tukio kama hili liligharimu maisha ya mgombea Ubunge wa Lushoto ndugu Mohamed Mtoi wiki chache zilizopita. Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi zinazoelezea mazingira ya kifo kilichompata Ndugu Mohamed Mtoi.
Kutokana na mfululizo wa matukio haya tunaliomba jeshi la Polisi lifanye Uchunguzi kujua namna gani kumekuwa na matukio kama haya yanayowapata wagombea Ubunge katika kipindi hiki cha kampeni. Pia wagombea Ubunge wote wachukue Tahadhari za kiusalama wanapokuwa katika harakati za kampeni kwa kuepuka kutembea safari za Usiku wanapokuwa katika kampeni, na pia kuwa na Ulinzi wa kutosha ili kuepuka matukio kama haya kuwakumba.



0 comments :
Post a Comment