
g
mafahali mawili tayari wmeshapiga kura
wagombea wakuu wa wanafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh john magufuli wa ccm na edward ngoyai lowasa tari wameshapiga kura. john magufuli amepiga kura yake akiwa huko jimboni kwake chato mkoa geita wakati lowasa amepiga kura huko jimbo la monduli mkoani arusha akiwa na mke wake.
TAARIFA YA CHADEMA/ UKAWA KUHUSU MWENENDO WA UCHAGUZI MKUU SIKU YA UPIGAJI KURA
2. Suala la watu wenye kadi lakini majina yao hayapo, ambapo kisheria inatakiwa msimamizi awape fomu namba 19 kisha waijaze na kupiga kura. Tumewataka wananchi kutokuondoka vituoni hadi wapate haki hiyo ya kujaza fomu hizo na kupiga kura.
Vifaa vya kupigia kura kuchelewa kufika vituoni ambapo baadhi ya vituo kama Kimara Temboni Dar es salaam, msimamizi amefungua kituo saa mbili kisha akasema karatasi za mgombea urais zimekwisha. Tumewataka wananchi katika maeneo kama hayo kutokuondoka vituoni, wakae kwa utulivu wahakikishe wanapiga kura.
Tumewataka NEC ambao wanapigiwa simu lakini hawapokei kutoa msaada wa haraka, wahakikishe suala hilo linatatuliwa haraka. Uchaguzi huu haukuwa ajali au suala la kushtukiza.
3. Idadi ya wapiga kura kwenye kituo kimoja kuwa kubwa tofauti na matakwa ya kisheria, kuna vituo tumebaini vinawapiga kura zaidi ya 800. Hairuhusiwi. Wapiga kura hawapaswi kuzidi 450 kwa kila kituo.
4. Madai ya kuwepo kwa kura feki kukamatwa katika maeneo mbalimbali zikiwa tayari zimepigwa, mfano tunazo taarifa za kukamatwa huko, Vunjo, Njombe na maeneo mengine ya nchi.
Hili tulitarajia tume ilizungumzie kwa udharura lakini mpaka sasa tunawatafuta watu wa tume hawapatikani.
Tunawahimiza watu wawe watulivu wasiondoke vituoni mpaka wapige kura ambayo ni haki yao kikatiba.
Tumaini Makene
Mkuu wa idara ya mawasiliano
CHADEMA
TAARIFA YA CCM KUHUSU MWENENDO WA WA UCHAGUZI SIKU YA KUPIGA KURA
ESTER NICHOLAUS MATIKO AIBUKA KIDEDEA HUKO TARIME MJINI
Mshindi amepata kura zaidi ya elfu ishirini na mshindi wa pili mgombea ubinge wa ccm amepata kura elfu kumi na nne

CCM KIDEDEA MAFINGA NI CCM. MGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA YA CCM JIMBO LA MAFINGA COSATO CHUMI AMESHINDA.
MSHINDI WA MAFINGA MJINI WAKATI WA KAMPENI (HAPO JUU)
JIMBO LA KAHAMA MJINI MGOMBEA UBUNGE WA CCM NDUGU JUMANNE KISHIMBA AMPIGA MWEREKA NDUGU JEMSI LEMBELI WACHADEMA BAADA YA KUPATA KURA ZAIDI YA 45000 HUKU LEMBELI AKIPATA KURA TAKRIBAN 30000
TUNDUMA MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA AIPATIA CCM MAUMIVU MAKALI BAADA YA KUIONGOZA CHAMA CHAKE KUPATA USHINDI MKUBWA KWA KUSHINDA UBUNGE NA VITI VINGI VYA UDIWANI.
NI HUSSEIN BASHE WA CCM HUKO NZENGA. MGOMBEA WA CHADEMA AGOMA KUSAINI FOMU ZA KUKUBALI MATOKEO. CCM PIA IMEPETA UPANDE WA MADIWANI KWA KUPATA KATA NYINGI
GEITA MJINI NAPO CCM YATWANGA. CHADEMA YAUMIA VIBAYA BAADA YA MGOMBEA WA CCM CONSTANTINE JOHN KANYANSU KUSHINDA UBUNGE NA VITI VYA UBUNGE
MONDULI CHADEMA YAPETA BAADA MGOMBEA WAKE NDUGU JULIAS KALANGA KUIONGOZA CHAMA CHAKE HICHO KUJIPATIA USHINDI MKUBWA KWA NAFASI ZOTE IKIWAMO YA URAIS UBUNGE NA UDIWANI.
NGOME YA CHADEMA MUSOMA MJINI YATEKWA JISOMEE MWENYEWE·
-Vedatus Mathayo (CCM) 32,836-Vincent Nyerere (CHADEMA) 25,549.
-Kati ya kata 14, CCM wamepata kata 12, CHADEMA kata 1 na CUF kata 1.
BABATI MJINI NI PAULINA GEKUL WA WA CHADEMA NA SIHA NI DR GODWIN MOLLEL WA CHADEMA PIA.
SINGIDA MJINI CCM WASHINDA BAADA MGOMBEA WAKE RAMADHANI SIMA KUTANGAZWA KUWA MSHINDI
ILEMELA ANGELINA MABULA WA CCM AWA MBUNGE KWA KUMSHINDA WAGOMBEA WENZAKE WALIOKUWA WAKIONGOZWA NA WA CHADEMA

0 comments :
Post a Comment