KIFARU ASAFIRISHWA KM 16000 AKZALISHE

faru asafirishwa kilomita 16,000 akazalishe 

Kifaru dume mmoja amesafirishwa umbali za kilomita 16,000 kutoka Marekani hadi Indonesia ili akazalishe.
Kifaru huyo kutoka Sumatra, ambaye vifaru wa aina yake wamo katika hatari ya kuangamia, amekuwa akiishi katika kituo cha kufugia wanyama pori Marekani.
Mnyama huyo aliyepewa jina la Harapan alizaliwa katika kituo cha kufugia wanyama cha Cincinnati, na ndiye kifaru pekee wa Sumatra aliyekuwa amebaki akiishi katika mataifa ya magharibi.
Wahifadhi wa wanyamapori wanatumai atajamiiana na vifaru jike katika mbuga moja ya kitaifa Indonesia.
Harapan
Vifaru wa Sumatra wamo hatarini kutokana na kuharibiwa kwa misitu na uwindaji haramu. Watafiti wanasema wamesalia vifaru chini ya 100 wa Sumatra mwituni.
Harapan mwenye umri wa miaka minane, ambaye jina lake linamaanisha matumaini, alisafirishwa kupitia ardhini, angani na majini hadi hifadhi ya vifaru katika mbuga ya wanyama ya Way Kambas.
 
Alisafirishwa kwa lori hadi bandarini na mwishowe akabebwa na feri hadi Sumatra
Dadake, Suci, aliishi naye katika kituo cha kufugia wanyama cha Cincinnati lakini aliugua na kufariki mwaka jana.
Vifaru wa Sumatra ndio wadogo zaidi na ndio pekee kutoka Asia ambao huwa na pembe mbili. Huwindwa sana na majangili kwa sababu pembe zao hutumiwa kutengeneza tiba ya kiasili Uchina.
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment