UPDATES KUWASILI KWA PAPA FRANCIS NCHINI KENYA

  1. PAPA AMEMALIZA KWA KUWASHUKURU TENA WAKENYA 
  2. PAPA ANAWAAMBIAVIONGOZI KUWA NI VIZURI KUWEKEZA KWA VIJANA KWANI VIJANA NI NGUVU KAZI AMBAYO INAHITAJI KUTUMIKA NANDIO WAJENZI WA TAIFA
  3. PAPA ANASEMA VIONGOZI SERIKALI WATENDE HAKI KWA RAIA WOTE
  4. PAPA ANSEMA KUWA MATUMIZI BORA YA RASILIMALI ZA ASILIAMBAZO MUNGU  AMEIJALIA KENYA NDIYO NJIA PEKEE ITAKAYOHAKIKISHA USAWA KENYA, PIA ANASEMA UBINADAMU NA USAWA NI NJIA NZURI YA KUHAKIKISAH KENYA INAFANIKIWA
  5. PAPA ANAANZA KWA KUMSHUKURU RAIS NA WAKENYA KWA UKARIBISHO NA UKARIMU WALIOUONYESHA. ALIPOFIKA
  6. RASI UHURU KENYATA ANAMKARIBISHA PAPA SASA
  7. RAIS ANAMWOMBA PAPA KUMWOMBEA YEYE MWENYEWE NA KENYA ILI MUNGU AWASIKIE 
  8. RAIS UHURU KENYATA ANASEMA ELIMU BORA INAYOTOLEWA NA KANISA IMEIFIKISHA KENYA KWENYE MAFANIKIO MAKUBWA. NA ANASEMA YEYE MWENYEWE NI MFANO WA MTU ALIYEFAIDIKA NA ELIMU KATIKA SHULE ZA KANISA KATOLIKI
  9. ANAISHUKURU KANISA KATOLIKI KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUTOA HUDUMA MBALI MBALI ZA KIJAMII KAMA AFYA NA ELIMU
  10. ANASHUKURU VIONGOZI WA DINI KWA JUHUDI KUBWA WALIYOWEKA KUIJENGA KENYA YENYA UMOJA
  11. ANASEMA PIA WAKENYA WAMEGAWANYWA NA UKABILA NA UDINI
  12. RAIS UHURU KENYATA ANAMSHUKURU BABA MTAKATIFU KWA KUANZA ZIARA YAKE NCHINI KENYA. NA ANAMWELEZA PAPA KUWA WAKENYA WANAYOFURAHA NA MSISIMKO MKUBWA KWANI WANAKABILIWA NACHANGAMOTO KAMA RUSHWA NA UGAIDI. RAIS ANAMWOMBA PAPA KUWAOMBEA WAKENYA KUSHINDA VITA DHIDI YA UFISADI NA UGAIDI
  13.  PAPA NA MWENYEJI WAKE BABA MTAKATIFU FRANCIS WANARUDI UKUMBINI
  1. RAIS WA ZAMANI WA KENYA NDUGU DANIEL ARAP MOI ANAINGIA UKUMBINI PAMOJA NA MWAI KIBAKI 
  2.  PAPA SASA AMEINGIA IKULU YA NAIROBI KWA MAZUNGUMZO NA RAIS UHURU KENYA;BAADA MUDA MFUPI ATAHUTUBIA WAKENYA MOJA KWA MOJA
  3. PAPA SASA ANAPANDA MTI WA KUMBUKUMBU
  4. 7:44 Papa Francis anapigiwa mizinga 21 ambayo kawaida hutumiwa kulaki kiongozi wa taifa jingine. Papa Francis ndiye kiongozi wa Vatican.
  5. 17:40 Papa Francis awasili Ikulu, Nairobi na kulakiwa na Rais Uhuru Kenyatta.
  6. 17:28 Rais Kenyatta amewasili ikulu ya Nairobi. Papa Francis yuko njiani kuelekea huko ambapo atakaribishwa rasmi Kenya.
  7. 17:25 Hivi ndivyo Papa Francis alivyoandika kwenye kitabu uwanja wa ndege wa JKIA: "na maombi na shukrani kwa kuwatunza wasafiri."
  8. Haya ni kwa mujibu wa Nexus Kenya, idara ya habari ya serikali ya Kenya.
  9. 17:15 Papa Francis aingia kwenye gari lake na kuondoka.
  10. 17:09 Wageni wanajiandaa kuondoka uwanja wa ndege wa JKIA. Papa Francis anatarajiwa kuelekea Ikulu kukaribishwa rasmi nchini na Rais Kenyatta.
  11.  
  12.  
  13. 16:52 Alakiwa kwa shangwe na nderemo. Amsalimia Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
    16:50 Wanahabari walioandamana na Papa Francis watangulia kushuka kutoka kwenye ndege.
    16:41 Viongozi wa Kanisa Katoliki wakiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wamejiandaa kumlaki Papa Francis atakaposhuka kutoka kwenye ndege iliyombebea, ambayo ni kutoka shirika la ndege la Italia, Alitalia.
    16:33 Ndege iliyombeba Papa Francis yatua uwanja wa ndege wa JKIA, Nairobi.
    16:25 Ndege iliyombeba Papa Francis kwa sasa imo kwenye anga ya Kenya.
    16:25 Rais Kenyatta ameelekea uwanja wa ndege wa JKIA kumlaki Papa Francis ambaye anatarajiwa kuwasili wakati wowote baada ya saa kumi unusu alasiri.
    16:20 Mabango yamewekwa katika barabara mbalimbali kumkaribisha Papa Francis Kenya
    16:08 Papa Francis aandika kwenye Twitter: "Mungu abariki Kenya".
    15:07 Papa Francis amezungumza na wanahabari walioandamana naye kwenye safari ya ndege kutoka Roma kuelekea Nairobi.
    “Ninaenda Kenya, Uganda na kwa ndugu zangu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati nikiwa na furaha,” shirika la habari la Reuters limemnukuu akisema.
    Image copyright AP
    “Tutumai kuwa ziara hii itazalisha matunda mema, kiroho na kimwili.”
    Image copyright Reuters

    12:36 Huyu hapa ni Papa Francis akiabiri ndege. Ndege yake ishaondoka uwanja wa ndege wa Fiumicino, Roma kuelekea Nairobi Kenya.
    12:11 Wakenya wanaendelea kujiandaa kumpokea Papa Francis baadaye leo. Barabarani na katika majumba, kuna mabando ya kumkaribisha Papa.
  14. Bofya hapa kusoma ratiba ya Papa Francis ziara yake Afrika
10:47 Magazeti ya Kenya yalivyoandika kuhusu ziara ya Papa Francis.










10:39 Makundi mbalimbali yamekuwa yakijiandaa kumlaki Papa Francis. Mfano ni watoto hawa kutoka kanisa la St Martin.




Hii hapa nayo ni kwaya ya pamoja ambayo itamwimbia Papa Francis.

10:33 Ndege ya Papa Francis imepaa kutoka uwanja wa ndege wa Fiumicino, Roma, ikiwa imechelewa kwa karibu robo saa. Anatarajiwa kuwasili uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta saa 17:00.
10:00 Hujambo! Karibu tukupashe yanayojiri katika ziara ya Papa Francis barani Afrika ambayo itamfikisha Kenya, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati.



















Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment