TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya
kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya
kumsikitisha.Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa
wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya
kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta
mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa
kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili
sasa, ilihalimashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya
kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko. Katibu Mkuu
Kiongozi BaloziOmbeni Sefue amesema na kutoa maelekezo yafuatayo:
Rais amevunja Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo
ilishamaliza muda wake na amemteua Prof. Lawrence Mseru , kukaimu nafasi
ya Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili kuanzia kesho tarehe 10 Novemba, 2015.
Dkt. Hussein L. Kidanto ambaye ndiye anayekaimu hivi sasa, amehamishiwa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambako atapangiwa kazi nyingine.
Balozi Sefue pia amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi
ya wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine
zote za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na
kuhudumia wananchi kama ipasavyo. Tayari Wizara ya Fedha imetoa shilingi
bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo na kulipa madeni ya ukarabati wa
mashine za uchunguzi wa magonjwa nchini.
Hata hivyo Katibu Mkuu
Kiongozi amesema kuanzia sasa hospitali zote nchini zinatakiwa kutenga
fedha kutoka kwenye mapato yao wenyewe na kuhakikisha mashine na vifaa
vyote vya kazi vinafanya kazi wakati wote (Regular Maintenance).
Balozi Sefue pia metumia nafasi hii kuwaagiza watendaji na viongozi wote
katika sehemu za kazi kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo na
kazi za umma zinatekelezwa ipasavyo. Hakutakuwa na huruma kwa watumishi
wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao Amesisitiza Balozi Sefue.
Mwisho
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu Dar es Salaam.
9 Novemba, 2015
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment