- kuongezeka kwa viti vya ubunge majimboni. kwa ujumla mpaka sasa wapinzani wanaongoza majimbo 71 kati 264 ambapo ukawa wana viti 70 kati ya hivyo CHADEMA wana viti 34, CUF majimbo 35 na NCCR mageuzi jimbo moja. pia chama kipya cha ACT wazalendo kilipata jimbo moja. Hili ni fanikio kubwa kwa wapinzani kwa kuwa wameongeza idadi yao ukilinganisha na uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo wapinzani walikuwa na majimbo machache kiliko haya ya mwaka huu
- wapinzani kuongoza majiji 4 kati ya 5 ni pigo lingine kwa chama tawala kwani majiji ni maeneo muhimu kiutawala, kiuchumi, kisiasa na kijamii. wapinzani wameshika hatamu ya utawala katika jiji la Arusha, Dar-es Salaam, Tanga na Mbeya na kuiachia CCM jiji moja tu la Mbeya
- Kuongezeka kwa Viti maalum vya Upinzani. ongezeko hili limepunguza idadi ya viti maalum vya CCM kuto 79 hadi kufikia 64. ongezeko hili vile vile limeongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni na ruzuku kwa vyama vyao.
- kupungua kwa ruzuku ya CCM na kuongezeka kwa ruzuku ya wapinzani kutokana na ongezeko la kura za Urais na wabunge
- kuongezeka kwa halimashari zinazoongozwa na upinzani kutoka 5 hadi kufikia halmashauri zaid ya 20
- kuongezeka kwa idadi ya wabunge wa upinzani kutoka 90 katika bunge la 10 hadi kufikia 117katika bunge lijalo la 11
WALICHOPATA UPINZANI KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
Hatimaye Uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani umekamilika kwa kiasi kikubwa. Pande za zilizoshiriki ucaguzi huo zimevuna walichokipanda kulingana na walivyozichanga karata zao. katika makala hii nimeorodhesha mafanikio ya upinzani ulioongozwa na vyama vinavyounda ukawa yaani CHADEMA, CUF, NLD na NCCR Mageuzi na chama kipya cha ACT Wazalendo. baadhi ya mafanikio haya ni
0 comments :
Post a Comment