Jana mamia ya wananchi wa jiji la mwanza walijumuka katika uwanja wa furahisha kwa lengo la kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa geita Hayati Alphonce Mawazo. Katika Kusanyiko hilo Viongozi wa Kitaifa wa chadema na ndugu jamaa na marafiki wa Marehemu walitoa matamko mbalimbali. baadhi ya matamko hayo ni haya hapa chini;
LOWASA
Amesema polisi wasipochukua hatua kwa waliomuua marehemu Mawazo watajichukulia hatua wao.
“Hawa Polisi wanafanya mambo yao kiimla-imla, kiujanja ujanja, wao
wameleta magari ya washawasha yaliyonunuliwa kwa Dola za Kimarekani 282
milioni, hawana namna ya kuyatumia, wameamua kuwachokoza wananchi ili
waweze kuyatumia.
“Wananchi nawaomba sisi tuache vurugu ili sasa
hayo magari yao walionunua tuone watakavyo yatumia, wananunua magari alafu
shuleni hakuna madawati na barabara hakuna,” amesema Lowassa.
MBOWE
“Wananchi wamechoka kuuliwa kama ilivyotokea kwa wafuasi wa Chadema
tangu mwaka 2011 mpaka sasa wakati huu wa Mawazo…tumechoka kufa, mwenye
akili na afahamu,”
“Kamanda Mkumbo lazima alipe gharama zote za siku nane za kumweka
Lowassa, Sumaye, Mbowe na wabunge zaidi ya 50 jijini Mwanza wakisubiri
mahakama itende haki na hatimaye kushinda kesi,” amesema mwenyekiti
Mbowe.
SUMAYE
“Kamanada Mkumbo lazima alipe gharama zote za siku nane za kumweka
Lowassa, Sumaye, Mbowe na wabunge zaidi ya 50 jijini Mwanza wakisubiri
mahakama itende haki na hatimaye kushinda kesi,” amesema mwenyekiti
Mbowe.
Sumaye amesema Marehemu Mawazo alikuwa akidai haki majukwaani, lakini
watu waliotaka kudaiwa haki waliamua kumuua huku vyombo vya dola
vikipindapinda ili haki isipatikane kwa amani.
“Lazima tusimamie amani na tupinge kuonewa maana ipo simu moja watu watachoka kuonewa kama ilivyo sasa,”
MTOTO WA MAWAZO PRECIOUS MAWAZO
“Wakati wa uhai wa baba, ndoto yangu ilikuwa niwe mwanasiasa, lakini
nitaendelea na hiyo ndoto hadi niwe mwanasiasa mkubwa nchini…katuacha na
mdogo wangu akiwa na miaka miwili tunaamini Mungu atatusaidia,”
GODBLESS LEMA
"ukimya wa wananchi katika mauaji wanayofanyiwa, si uoga
bali ni unatokana na uchungu walionao, kwani wauaji wakiwa huru hakuna
atakayekuwa salama".
MCHUNGAJI SWAI WA KANISA LA THE WINNERS
“Lazima wanadamu wajiulize kwanini vijana wengi wanatumiwa ili kuwaua
wengine, tunaiomba serikali iliyopo madarakani isimamie na kukomesha
kabisa mauaji yasiyo na hatia,”
"Binadamu hawajaumbwa kwa ajili ya kuuana bali kwa ajili ya kupendana"
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment