Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta uozo . Maafisa hao wametakiwa kusalimisha hati zao za kusafiria, na hii imekuja baada ya kugundulika kuwa kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.
Katika Ziara hiyo ya ghafla Waziri
mkuu Kasim Majaliwa awasimamisha kazi kamishna wa kodi Tiagi Masamaki na
Habibu Mpozya kitengo cha huduma kwa wateja kutokana ubadhilifu wa
fedha kwa makontena zaidi ya 300 yaliyopotea.
Wengine ni Haruni Mpande -ICT, Hamisi Ali Omari na Eliachi Mrema incharge wa ICD na amemuru wote wakamatwe uchunguzi uendelee.
Wengine ni Haruni Mpande -ICT, Hamisi Ali Omari na Eliachi Mrema incharge wa ICD na amemuru wote wakamatwe uchunguzi uendelee.
0 comments :
Post a Comment