ZAIDI ya vijana
50 wa CCM Iringa Mjini wanaojiita “wafia chama”, kwa zaidi ya saa mbili juzi
waliwafungia ndani ya ofisi za CCM Mkoa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa
akiwemo Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu
anayeshinikizwa aachie ngazi.
Msambatavangu anatuhumiwa na baadhi ya makada wa chama hicho kukihujumu katika Jimbo la Iringa Mjini wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu jambo lililosababisha kupoteza kata 14 kati ya 18, ikiwa ni pamoja na kupoteza jimbo hilo kwa mara nyingine kwa mbunge wa Chadema, Mchungaji Peter Msigwa.
Akizungumzia tuhuma wanazomhusisha nazo Msambatavangu; mmoja wa vijana hao, Salum Mbungu ambaye ni Katibu wa Vijana Kata ya Ruaha na Katibu wa Makatibu wa Vijana wa kata zote 18 za jimbo la Iringa Mjini, alisema:
“Tunataka Mwenyekiti wa Mkoa ajiuzulu kwa hiari yake, kuna ushahidi tosha unaomhusisha yeye binafsi na baadhi ya vijana wa CCM kukihujumu chama wakati wa Uchaguzi Mkuu.”
Mbungu alidai wanao ushahidi unaoonesha kiongozi huyo alikuwa akiwashawishi baadhi ya wanaCCM kuwachagua wagombea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa sababu alikuwa mpiga debe maarufu wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa wakati akiwa katika mchakato wa kuwania urais kupitia CCM.
Akizungumzia tukio hilo baada ya vijana hao kuombwa kutawanyika huku wakihakikishiwa hoja zao zinafanyiwa kazi katika vikao husika, Msambatavangu alisema hatajiuzulu na kwamba tuhuma zinazotolewa na vijana hao na wanaCCM wengine dhidi yake si za kweli, zinalenga kuchafua hadhi yake na kuficha ukweli wa sababu zilizosababisha wapoteze jimbo hilo.

0 comments :
Post a Comment