Michezo ya mzunguko wa pili wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports
Federation Cup) inaendelea leo katika viwanja vitatu tofauti, huku kila
timu ikisaka ushindi na kuweza kusonga katika hatua inayofuata
itakayochezwa mwakani Januari, 2016 na bingwa kuwakilisha nchi mwaka
2017 katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CC).
Leo katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, African Lyon
watawakaribisha Ashanti United, mjini Tabora Polisi Tabora watacheza
dhidi ya Rhino Rangers na uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Sabasaba FC
watawakaribisha Burkinfaso FC.
Kesho Jumatano kutachezwa michezo miwili, Friends Rangers
watawakaribisha KMC katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, huku
katika uwanja wa Sheihk Amri Abeid jijini Arusha, Madini FC watacheza
dhidi ya maafande wa JKT Oljoro.
Alhamisi michuani hiyo itaendelea kwa michezo mitatu, Panone FC
watawakaribisha Kiluvya FC uwanja wa Ushirikia mjini Moshi, Lipuli FC
watacheza dhidi ya Kurugenzi uwanja wa Wambi – Mafinga, huku Mbao FC
wakiwakaribisha Geita Gold kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment