JAPO HAWACHEZI WAO KWA WAO YANGA NA AZAM LEO WATAPIGANA KUFA KUPONA ILI KUKALIA USUKANI WA LIGI

Image result for yanga VS Image result for AZAMAZAM FC inamenyana na Majimaji Uwanja wa Majimaji mjini Songea leo katika mchezo ambao ikishinda inarejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Azam FC ilishushwa kileleni na mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumatano.
Lakini leo Azam FC inakutana na Majimaji ambayo mchezo wa mwisho ilifungwa 5-1 na vibonde wenzao Toto Africans Uwanja wa Majimaji.
Azam FC inapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa leo na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, kutokana na ukweli kwamba Majimaji ni timu dhaifu.
Mabingwa watetezi, Yanga SC nao pia watashuka dimbani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kumenyana na Stand United ya Shinyanga, ambayo hakika na timu ngumu.
Ikitoka kufungwa 2-0 nyumbani na Mwadui katika mchezo wake uliopita, Stand inayoongozwa na kinara wa mabao wa Ligi Kuu, Elias Maguri inatarajiwa kupambana leo kuzinduka.
Nao mabingwa wa zamani wa ligi hiyo, Simba SC watakuwa Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza leo kumenyana na Toto Africans. 
Toto imekuwa na kawaida ya kuifunga Simba SC Uwanja wa Kirumba na hilo linafanya mchezo wa leo, uvute hisia za wengi. 
Simba SC leo wanatarajiwa kuwa kamili, baada ya wachezaji wake iliyowaingiza dirisha dogo, Mganda Brian Majwega, Mkenya Paul Kiongera na wazalendo Novat Makunga na Hajji Ugando kuruhusiwa kucheza.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo ni kati ya Mwadui FC na Ndanda FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Kagera Sugar na African Sports Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora na Prisons na Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya – wakati kesho JKT Ruvu wataikaribisha Coastal Union Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam na Mbeya City watakuwa wenyeji wa Mgambo JKT Uwanja wa Sokoine.

Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment