Kama unakumbuka: Post yangu iliyopita, niliandika kuhusu China kutuma chombo chao kwenda mwezini.
Chombo hicho kilifika salama na kuanza kazi zake; lakini sasa imeripotiwa kuwa chombo hicho kimekumbana na hitilafu, na kitazimika kwa siku zisizopungua kumi na nne (14).
Matatizo hayo yaliyoanza wiki iliyopita, bado haijajulikana vizuri yamesababishwa na nini.
Kama mnavyofahamu, Mwezi huzunguka katika kipenyo chake kwa siku 28. Na, kwa siku 14 huangazwa na Jua, lakini siku zinazobaki huambulia kivuli tu.
Sasa, Chombo hicho cha China kiitwacho Yutu, au ‘Jade Rabbit’ kwa Kingereza hutumia solar panel, kwahiyo hufanya kazi vizuri mwanga wa Jua unapokuwepo. Kipindi cha giza kinapoanza kwenye Mwezi; hali ya hewa hushuka hata kufikia nyuzi joto -170 °C. WanaSayansi wa China kwa kulijua hilo, walikiwekea chombo hicho mode ya ’Hibernation’ ili kuweza kujilinda na kuendelea kuwa hai.
Lakini sasa, tatizo lilitokea wiki iliyopita limekorofisha kabisa mode hiyo ya ’Hibernation’ katika chombo hicho. Na, sasa kipindi cha giza ndo kinaanza; kwahiyo kuna asilimia kubwa kwamba Chombo hicho kitakufa.

Chombo hicho, kwa huzuni kubwa leo kimetuma tweet iliyowaumiza wakazi wengi wa China. Tweet hiyo ilisomeka: “Leo, asubuhi ilibidi nianze usingizi wa muda mrefu, lakini waumbaji wangu wamegundua tatizo kwangu, na huu ndio unaweza ukawa mwisho wangu”.
Najua waweza kujiuliza Chombo kimetumaje tweet… usihofu; tweet hizo zimeandikwa na mmoja wa wadau wa chombo hicho.
Watu wengi wa China, leo wameonyesha umoja kwenye twitter, kwa huzuni, waki-tweet jumbe zenye hashtag (#Hang_In_there_Jade_Rabbit)…
Chombo hicho kilimaliza kwa kusema jioni hii: “I’ve said a lot, yet I feel like it’s not enough”. “Good Night, planet Earth. Good Night Humanity.”
Hatma ya chombo hicho itajulikana baada ya hizo siku 14, na tutajua kama kimekufa, au bado kipo hai…
Leo nimekuwa nikizifuatilia tweet za Chombo hiki kwa huzuni sana leo. Ninatumai, baada ya siku 14 bado kitakuwa hai.
Namalizia pia kwa kukiambia chombo hichi: #Hang_In_There_Jade_Rabbit

0 comments :
Post a Comment