KUMEKUCHA; WABUNGE NA MADIWANI WA UKAWA WILAYA KINONDONI WASEMA MKURUGENZI ALIYESIMAMISHWA ANAONEWA KWA SABABU ZA UCHAGUZI

LEO MADIWANI NA WABUNGE WA UKAWA MANISPAA YA KINONDONI
tumeiomba Ikulu (OFISI YA RAIS) iteue TUME HURU YA UCHUNGUZI "a free and independent inquirery Commission" dhidi ya tuhuma za mkurugenzi aliyesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zake 3,i/uduni wa ubora wa barabara zilizo jengwa manispaa yabkinondoni na kushindwa kuwaadhibu wahandisi wahusika
ii/kushindwa kusimamia idara ya ardhi na mipangomiji ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi,iii/kukosa uadilifu katika ubinafsishwaji wa fukwe za cocobeach
UKAWA MANISPAA YA KINONDONI,tumegundua kuhusishwa na siasa za baada ya uchaguzi,kwa kuwakomoa,kufitinisha na kuadhibu wakurugenzi walioshindwa kuzuia UKAWA tusitangazwe kwenye uchaguzi mkuu 2015,sasa kwakubambikiwa tuhuma na kuhusishwa na ufisadi au uzembe......pia tumekiri ambapo tume itagundua mkurugenzi alikuwa na hatia ya ufisadi au uzembe pia awajibishwe kulingana na alichokitenda kwakuwa si dhumuni letu kutetea ubadhirifu au ufisadi
Tumekataa TAMISEMI kuhusika na hatua zinazofuata kwa uchunguzi kwakuwa wanajua kila kitu kinachoendelea katika UFISADI wa fukwe za COCOBEACH,kwakuwa ukweli wanaujua ila wameuficha na kumzunguka mheshimiwa Rais na kubambikia wengine.
TUMEUWEKA HADHARANI MAKATABA WA COCOBEACH,wananchi waone waliobinafsisha fukwe ya COCOBEACH 2007, NA Majina ya waliotia saini mkataba huo mwaka 2007,wakati mkurugenzi Eng MUSSA NATTY,Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa KINONDONI 2013.
Ukweli huu wa kusingiziwa swala la cocobeach uwe chachu ya Tume kutafuta ukweli halisi wa tuhuma zingine,kwa kuwa TAMISEMI walihusika kila hatua ya uuzaji wa fukwe hizo.
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment