LIGI KUU TANZANIA BARA YANGA MWENDO MDUNDO SIMBA YACHECHEMEA

KAM
Ligi kuu soka Tanzania bara imeendelea kwa mchezo mmoja ambao umepigwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga jana ukuzikutanisha Africans Sports na Yanga.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa vuta nikuvute wenyeji African Sports walionekana kucheza vyema dhidi ya Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara ambapo wenyeji walikuwa mara kwa mara wa Kifika langoni mwa Yanga lakini washambuliaji wake wakishindwa kumalizia.
Kipindi cha pili timu zote zilicheza kwa kujihami na kushambuliana kwa zamu ambapo katika dakika za majeruhi juhudi hizo zilizaa matunda kwa Yanga ambao kupitia kwa mchezaji Thaban Kamusoko alifunga goli la ushindi, ambalo linakuwa goli lake la pili msimu huu.
Kwa matokeo hayo sasa Yanga imepaa kileleni mwa ligi hiyo kwa kufikisha jumla ya alama 27 ikifuatiwa na Azam yenye alama 26 na mchezo mmoja mkononi wakati Africans Sports wakisalia mwishoni mwa ligi hiyo kwa kuwa na lama 4.
Huko jijini mwanza simba imelazimishwa sare ya bao moja kwa moja. bao pekee la simba lilifungwa na Dany lyanga kipindi cha kwanza. Toto wasawazisha bao dakika za majeruhi za kipindi cha pili
Nao mwadui united imefanikiwa kubakisha pointi tatu nyumbani baada ya kuwafunga Ndada united bao 2;1
Mtibwa united na waliwalazimisha wajelajela wa prison sare. na hivyo timu hizo kumaliza dakika 90 kwa kugawana pointi
kagera sugar walifanikiwa kuondoka na pointi tatu muhimu baada ya kuwatungua wapinzani wao wa african sports kutoka jijini tanga
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment