TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU ZIARA YA MH. EDWARD LOWASSA KUSHUKURU WATANZANIA
Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania kwa
ujumla kuwa aliyekuwa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA), Ndugu Edward Lowassa atazungumza na wananchi wa Tanga
katika mkutano wa hadhara utakaofanyika mjini Tanga, siku ya Alhamis,
Desemba 17, 2015.
Mkutano huo ni sehemu ya ziara ya viongozi
waandamizi wa Chama na UKAWA kwa ujumla ambao watakwenda maeneo
mbalimbali nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa namna walivyounga mkono
upinzani na agenda nzima ya MABADILIKO katika uchaguzi mkuu uliopita na
wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani kuwa ndiyo nguzo imara
wanayoweza kuitegemea kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya
maendeleo yao na ustawi wa taifa kwa ujumla.
Itakumbukwa kuwa
mbali ya Watanzania kupiga kura za ushindi katika nafasi ya urais katika
uchaguzi mkuu uliopita, wananchi waliwachagua wabunge wengi wa upinzani
wanaotokana na UKAWA na kuongeza nguvu kubwa ndani ya bunge hususan
kupitia Kambi ya Upinzani Bungeni ambayo itakuwa serikali yao mbadala
huku wakiviamini vyama hivyo kusimamia na kuongoza halmashauri zipatazo
34 nchi nzima, ikiwa moja ya misingi imara katika kupigania mabadiliko
ambayo Watanzania wanayataka.
Wananchi wanastahili shukrani kwa
imani hiyo kubwa ambayo ni ishara ya wazi kuwa matumaini yao kwa miaka
mingine mitano yatasimamiwa na kuongozwa na upinzani imara kupitia
UKAWA.
Katika ziara hiyo ya Tanga, Ndugu Lowassa ataambatana na
viongozi wengine waandamizi wa UKAWA ukiwa ni mwanzo tu wa ziara kubwa
itakayokwenda nchi maeneo mbalimbali nchi nzima.
Imetolewa leo Jumanne, Desemba 15, 2015 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment