MATOKEO YA LIGI KUU BARA LEO JUMAPILI DECEMBA 20/2015

Image result for azam fc
Azam FC imezidi kujichimbia katika nafasi ya pili baada ya kuongeza pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu Bara.

Azam FC imeongeza pointi hizo baada ya kuitwanga Majimaji kwa mabao 2-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Kikosi hicho cha Azam FC kilipata mabao yake mawili katika kipindi cha kwanza kupitia Ame Ali na Didier Kavumbagu katika dakika za 10 na 20.

Hata hivyo hali ya uwanja ilikuwa hovyo kutokana na mvua zilizonyesha mchana kutwa.

Mara kadhaa, mpira ulikwama kwenye madimbwi kutokana na maji na matope kujaa uwanjani.

Kwa ushindi huo, Azam FC unefikisha pointi 29 nyuma ya Yanga iliyo kileleni ikiwa na pointi 30.
Nao mbeya city wameshindwa kutumia uwanja wao wa sokoine mjini mbeya baada ya kulazimishwa sare na mgambo shooting ya tanga

Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment