MBOWE; HATUTAMPINGA MAGUFULI KWA KILA JAMBO ILA KWA PALE ATAKAPOFANYA........

Image result for mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema kuwa wao kama wapinzani hawatapinga kila jambo litakalokuwa linafanya na Serikali ya awamu ya tano.

Amesema kazi yao ni kuisimamia Serikali, watakuwa wanapinga kwa hoja za msingi, pia amesema baadhi ya mambo ambayo wao wameyapigia kelele kwa miaka mingi vinatekelezwa sasa na Rais Magufuli, japokuwa sio kwa usahihi.

Amepinga teuzi mbili katika baraza la Mawaziri, amepinga uteuzi wa Waziri wa Katiba na Sheria na uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo kwani wananuka rushwa

Amesema kuwa Dkt. Mwakyembe anahusika na madudu ya bandarini na Bodi ya Bandari iliyovunjwa na Rais Magufuli kwa asilimia kubwa iliteuliwa na Dkt. Mwakyembe.

Pia amesema Prof Muhongo alijiuzulu kwa shinikizo la maazimio ya Bunge, inashangaza anateuliwa hata kabla ya mwaka kukamilika tangu awajibishwe na Bunge.


Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment