MBUNGE
wa Viti Maalumu mkoa wa Mara, Joyce Sokombi kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amempongeza Rais John Magufuli, kwa
kasi yake ya kuwawajibisha watu na
watumishi wa serikali wanaojinufaisha na mali ya umma.Mbunge huyo
alisema kasi ya Rais Magufuli inaridhisha kwa kuwawajibisha watu na
watumishi wa serikali wanaohujumu mali za umma na kwamba Chadema, siku
zote imekuwa ikisisitiza watu kuwajibika kwa kufanya kazi halali na siyo
kuhujumu mali za umma kwa manufaa yao binafsi.
Sokombi aliyasema hayo jana mjini Bunda wakati akizungumza na wenyeviti na makatibu wa chama hicho katika majimbo ambayo Chadema iliyapoteza katika Uchaguzi Mkuu uliopita ambayo ni Mwibara, Butiama, Musoma, Bunda na Musoma Vijijini, Kikao ambacho kilikuwa ni kwa ajili ya kufanya tathmini ya uchaguzi huo.Alisema siku zote kaulimbiu ya Chadema ni watu kufanya kazi halali na siyo kuiba mali za umma kwa maslahi yao binafsi na kwamba sasa uchaguzi umekwisha kinachotakiwa kwa wananchi wa mkoa wa Mara ni kufanya kazi za kujiletea maendeleo na sio kuiba na kujinufaisha na mali ya umma.
“Siku zote sisi Chadema tumekuwa tukipinga ufisadi na wizi wa mali ya umma, kinachotakiwa ni kufanya kazi halali na siyo kuiba na kujinufaisha na mali ya umma… uchaguzi umeisha wananchi sasa tufanye kazi za kujiletea maendeleo,” alisema.

0 comments :
Post a Comment