MWANAMFALME WA SAUDIA AMSHUTUMU DONALD TRUMP, DONALD NAYE AJIBU MAPIGO ASEMA MWANAMFALME NI MJINGA

TalalaMwanamfalme Alwaleed bin Talal wa Saudi Arabia amemshutumu mgombea urais wa chama cha Republican Marekani Donald Trump kwa tamko lake kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.
Mwanamfalme huyo, ambaye ndiye mtu tajiri zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu, amesema Bw trumo anafaa kuacha azma yake ya kutaka kuwa rais kwa sababu hawezi kushinda.
"Unaletea aibu chama cha Republican na Marekani kwa jumla," ameandika Bin Talal kwenye Twitter.
Bw Trump, mfanyabiashara tajiri kutoka New York, alikuwa amependekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani kwa sababu za kiusalama.
Hii ni baada ya wanandoa wawili Waislamu kufyatua risasi na kuwaua watu 14 mjini San Bernardino, jimbo la California.
Trump
Amejibu matamshi hayo ya Bw Talal kwa kumuita mwanamfalme ”mjinga” na kumtuhumu kwa kutaka kufanya anachosema ni kutumia “pesa za baba” kudhibiti wanasiasa wa Marekani.
"Hutaweza kufanya hivyo nikichaguliwa," amemjibu Trump kupitia Twitter.

Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment