SIMU FEKI ZOTE KUFUNGIWA.

Image result for nokia phones
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetoa miezi sita kwa watumiaji wa simu za mkononi ambao wanatumia simu bandia kuachana nazo la sivyo watazifungia.
Pia TCRA imetoa mwongoza kwa watumiaji wa simu hizo kuzihakiki simu zao kama ni halali, ambapo watumiaji wanatakiwa kupiga simu*#06# harafu zitatokea namba mara baada ya kupiha na kinachotakiwa ni kuzichukua namba hizo kisha kwenda kwenye sehemu ya kuandika ujumbe mfupi na kuziandika namba hizo,
Halafu unatuma ujumbe wa namba hizo kwenda kwenye namba maalum 15090 na kutapata matokeo kamili kuhusu uhalali wa simu ikiwemo pia kuzisajili.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam mkurugenzi mkuu wa (TCRA) Dkt Ally Simba wakati akiutambulisha, mfumo mpya wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani, kwenye makao makuu ya Mamlaka hiyo yaliopo Jijini Dar es salaam,ambapo amesema nia ya TCRA ni kuziondoa simu zote bandi katika mfumo wa utumiaji wa simu.
Pia amesema mfumo huo utasaidia kuongeza usalama mtandaoni kwa watumiaji wa simu kwa madai kuwa simu zote za mkononi zitakuwa zimejulikana kutokana na kusajiliwa kwenye mfumo huo na kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango hivyo kusaidia kuepeka madhara yatokanayo na simu zisizokuwa bora stahiki.
Sanjari na hayo,Dkt Simba amesema mtumiaji wa simu atakuwa na uwezo wa kuripoti mara simu yake inapoibiwa na kuifanya isiweze kutumika na mtandao wowote wa simu hapa nchini na kupelekea kupungua wizi wa simu.
Kwa upande wake Katibu mkuu kiongozi,Ombeni Sefue ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa mfumo huo amewataka watanzania kuachana na tabia ya kutimia simu kwa matumizi ya uharifu.
“Hatuwezi kukubali kama serikali kukawa na watu wanatumia simu kwa matumizi ya kufanyia uharifu kutapele watu,kwa kweli tumechoka sasa nauhakika mfumo huu utasaidia kuwakamata watu hawa wanasumbua watanzania”amesema Sefue
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment