TP MZAMBE YAWA JAMVI LA WAGENI HUKO JAPAN

Image result for TP MAZEMBEImage result for TP MAZEMBE Mabingwa wa soka Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamecharazwa 2-1 na Club America ya Mexico katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia la Klabu.
Mechi hiyo ilikuwa ya kuamua nani angemaliza nambari tano katika fainali hizo ambazo zinachezewa Japan.
Dario Benedetto na Martin Zuniga walifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na kuwaweka mabingwa hao wa Concacaf kwenye udhibiti wa mechi hiyo.
Rainford Kalaba alikombolea mabingwa wa Afrika mechi moja zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mechi kuisha.
Lakini mabingwa hao hawakuweza kujikwamua na safari yao kwenye michuano hayo iliisha kwa masikitiko.
Kabla ya mechi hiyo, Mazembe walikuwa wamechapwa 3-0 na Sanfrecce Hiroshima kutoka Japan hatua ya robofainali, kwenye mechi iliyochezewa mjini Osaka Jumapili.
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment