
Kufuatia Kukamatwa Kwa Mbunge Wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) Jana Kwa Amri Ya Mkuu Wa Wilaya Kinondoni Paul Makonda Na Leo Kufikishwa Mahakama Ya Kisutu Na Kusomewa Shtaka La Kutoa Lugha Chafu Kwa Dc Huyo, Wanasheria Wa Chadema Wamesema kuwa watamshughulikia mkuu huyo wa wilaya kwa kutumia vibaya mamlaka yake.
TUNDU LISSU : (Mwanasheria Mkuu Wa Chadema) Alisema Mkuu Wa Wilaya Anayo Mamlaka Ya Kuamuru Mtu Aliyefanya Kosa Akamatwe Ikiwa Mahali Hapo Hakuna Polisi.
'Kama Kuna Polisi Kwenye Eneo La Kosa, Dc Hana Mamlaka Hayo, Na Kama Akitoa Amri Hiyo Anatakiwa Awajibike Kutoa Maelezo Na Sababu Za Kukamatwa Mtu Huyo Kwa Hakimu Wa Wilaya'.
Alichokifanya Dc Wa Kinondoni, Paul Makonda Ni Uvunjwaji Wa Sheria, Naapa Tutamshughulikia na Atakimbia Hiyo Wilaya' - Alisema Tundu Lissu.
MWANASHERIA PETER KIBATALA : Amesema Amefurahi Kutokea Kwa Kesi Hiyo Na Anaomba Swala Hilo Kwenda Mahakamani Kama Shtaka La Jinai.
Alisema Kesi Hiyo Itasaidia Kuhoji Mamlaka Ya DC Na Jinsi Anavyoyatekeleza.
0 comments :
Post a Comment