Habari ya mama aliyeuguliwa ghafla na mtoto wake majira ya SAA 2 usiku,
mtoto alibanwa na kifua(asthma), hali ilikuwa mbaya na mama akaenda
kuomba
msaada kwa jirani yake aliyekuwa na gari, akamjibu gari
haina mafuta, akaenda kwa mchungaji ili amsaidie, akamjibu nina
wachungaji toka USA, hivyo sitaweza kuwaacha peke yao, mama hakuwa na
jinsi aliamua kumbeba mtoto ili amuwahishe hospitali akiwa na hofu asije
kufa kama baba yake aliyefariki miaka michache kwa ugonjwa huo.
Huyo mama alikuwa na tatizo la mguu na mtoto alikuwa mzito, mama alianguka Mara kadhaa na akainuka kuendelea na safari.
Njiani alikutana na watu waliotoka kazini aliomba wamsaidie walimpuuza na alijaribu kusimamisha magari hayakusimama.
Kichaa mmoja mchafu aliyekuwa akizungukazunguka mitaani na jalalani
alipomuona yule mama anavyohangaika na mtoto akamwendea na kumchukua
mtoto, kisha akamweka begani, mama hakuwa na la kusema ila kumwelekeza
Hospitali, yule kichaa alielewa akaenda haraka hadi Hospitali.
Ma
doctor walipomuona yule kichaa na mtoto wakajua kuna dharura,
wakamchukua mtoto na kumhudumia haraka, baada ya dk.10, mama wa mtoto
akawasili, kisha ma doctor wakatoa taarifa kuwa, mtoto angecheleweshwa
dk 5 angekufa.
MUNGU alimtumia yule kichaa mchafu kuokoa maisha ya
mtoto. Hivyo usimteegemee Mch, jirani, wenye magari, matajiri nk. MUNGU
huweza kuinua MTU usiyemdhania kukubariki. Mwamini MUNGU atakubariki.
Usitumainie wanadamu hakuna baraka kwao. MUNGU huinua vinyonge ilI
kuangusha vyenye nguvu.
Hakika muwe na siku njema
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment