IMANI SI LELEMAMA

Utasikia watu, eti, watumie watu 10 utaingia peponi. Au mambo yako yatakuwa mazuri, hivi mnadhani Pepo mchezo!
Yohana mbatizaj aliishi hadi mapangon kwa kula asali na nzige kwa ajili ya kuitangaza injil,
Mtakatifu Yohana yule mwanafunzi wa Yesu, alikaangwa kwenye mafuta yanayochemka, baadae akatupwa kwenye kisiwa cha mateso cha patmo mpaka akafunuliwa mambo mazito na magumu
Isaya aliuwawa kifo cha kukatwa vipandevipande kwa msumeno wa kukatia mbao akiwa hai.
Stephano alipigwa kwa mawe mpaka akafa
Daniel alitumbukizwa kwenye tundu la simba sababu ya kuishindania imani, Yusuph ilimbidi kwenda gerezani kwa sababu ya kuulinda utakatifu wake, shedrack, meshack na abelnego walitumbukizwa kwenye tanuru liwakalo moto. Yote hii ni kwa sababu ya kuisimamia imani
Leo hii anatokea, mtu, kwa msg yake isiyo na mashiko wala vina alafu anakutisha, anakulazimisha utume kwa watu 10 maisha yako yatakuwa mazuri, au eti mm ni Yesu/Mtume Mohammad S.A.W nakuagiza tuma ndani ya dk 3.
Unadhani mbinguni ni kariakoo? kwa sms yako tu ukale bata mbingun, halafu unategemea uingie Peponi, tusidanganyane, Pepo sio mas'hara ndugu yangu, sio maneno matupu na sms nyingi.
Tumche Mungu kisawasawa.
WAKUMBUSHE WANAOGAWA PEPO KWA SMS..😂😂
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment