Mchezo
wa nusu fainali kombe la Mapinduzi kati ya Yanga SC na Simba SC
umemalizika kwa mikwaju ya penati na mnyama Simba SC akiibuka kidedea
kwa kupata 4-2.
Kwa
ujumla ni moja kati ya mechi bora za watani wa jadi kuwahi kutokea hivi
karibuni. Timu zote zikionesha nidhamu kubwa ya mchezo na ufundi mkubwa
idara zote.
Mechi
ya mzunguko wa kwanza ligi kuu Tanzania bara iliyomalizika kwa sare ya
1-1 ilitawaliwa na ugomvi mkubwa , kukamiana na kila aina ya karaha
hivyo mchezo wa kistaarabu leo umeonesha ukomavu kwa timu zote mbili .
Kimbinu na kiufundi
Tuanze
na washindi Simba SC. Mwalimu Joseph Omog aliipigia mahesabu Yanga SC
ya kuishambulia muda wote wa mchezo kwa kutumia nguvu kubwa ya viungo
wake . Akitumia mfumo wa 4-4-2 ambao mara nyingi katika eneo la kiungo
hutumia viungo wawili na sapoti ya mawinga kulia na kushoto kuwachezesha
washambuliaji wawili mbele, lakini leo Omog alijaza takribani viungo
sita . James Kotei akisimama chini sambamba na Jonasi Mkude , Mohamed
Ibrahimu juu , Muzamiru Yassin kama kiungo mshambuliaji na Luizio kama
target Man na Kichuya kulia . Wote hawa ni viungo akiwa na mahesabu ya
kumiliki mpira , kupanga mashambulizi pia kuikataa Yanga kucheza kati (
direct play )
Kwa
kiasi kikubwa Omog alifanikiwa na ndio maana Yanga walipakimbia kati
kwa kuweka mpira bali walitumia mipira mirefu kwenda mbele . Muunganiko
wa Juma Makapu , Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima ulikosekana na
muda mwingi mashambulizi yakijengwa kupitia pembeni kwa wing backs .
Heko za pekee kwa Besala Bukungu na Zimbwe Jr ambao leo walikuwa makini
kucheza na flanks kwa kupanda kwa tahadhari baada ya kugundua Yanga
wanatumia long balls pembeni kufika mbele .
Simba
SC ilishindwa kuamua matokeo ndani ya dakika 90 licha ya kuonekana
kuizidi Yanga eneo la kiungo kutokana na sababu zifuatazo kimbinu;
Muingiliano
wa James Kotei na Jonasi Mkude katika kuisukuma timu mbele . Walijikuta
muda mwingi wanasimama Sambamba na kuvunja ile link yao na Muzamiru
Yassin ambaye akajikuta leo anadhurura tu uwanjani . Kujipanga vibaya
kuliwafanya Makapu na Kamusoko wakisaidiwa Deusi Kaseke aliyekuwa
anavunjikia kati kuzima mipango yao ya kushambulia kitu ambao kilikuwa
kina mtesa Juma Luizia kupata mipira . Kotei alihitaji sana kuweka mpira
chini na kushambulia kwa kasi lakini wenzake walikuwa na tension kubwa
na kujikuta wanaingiliana . Kanikosha kwa mbinu zake .
Mpango
wa kupitia Pembeni ulikuwa mgumu kwa aina ya uchezaji wa Simba ambao
hawana Sprinters wazuri kwenye wings . Wanahitaji give and go passes
kwenda mbele .
Lakini
pia kukosa utulivu kwenye final third kumeigharimu Simba . MO Ibrahimu ,
Muzamiru na Juma Luizio walikuwa wanafika langoni bila mipango pia
uchoyo na papara za kufunga . Viungo wa kati kucheza nyuma sana
kuliwafanya viungo na walinzi wa kati wa Yanga kuelewana vyema na kuzuia
" pressing " mahesabu ambayo Omog aliyahitaki sana kwa kujaza viungo.
Tukija
kwa Yanga SC nitoe kongole kwa benchi la ufundi la Yanga SC kwa
kuifanyia mabadiliko makubwa timu hiyo baada ya kupoteza 4-0 dhidi ya
Azam FC . Mabadiliko kimbinu na kiufundi.
Yanga
leo imeonesha nidhamu kubwa ya mchezo kwa dakika zote 90. Kitendo cha
kuiheshimu Simba na kuichukulia tahadhari ndio kimewapelekea kutoka
salama ndani ya dakika 90 na kwenda kupoteza kwenye matuta.
Mechi na Azam FC tatizo kubwa lilikuwa nafasi ya kiungo , ulinzi na jinsi ya kujipanga golikipa .
Hakukuwa
na uelewano mzuri kati ya Andrew Vicent na Kelvin Yondani . Kukatika
kwa Zullu na wenzake pia usimamaji mbovu wa Dida langoni kulipelekea
maafa.
Mechi
ya leo kumekuwa na uelewano mzuri kati ya Dante na Yondani
wakiunganishwa vyema Juma Makapu kama deep lying holding midfielder.
Uelewano wao uliwafanya washambuliaji na viungo wa Simba kushindwa
kuwapita na kuwasukuma nyuma licha ya wingi wao . Heko kwa Yondani kwa
kucheza jihadi hasa kama mtu wa mwisho kwenye marking.
Dida
ameokoa magoli ya wazi matatu kwa kujipanga vyema langoni mwake leo .
Alikuwa muda mwingi anachukua tahadhari kabla ya mpira kumfikia kitu
ambacho kimemfanya kuwa bora leo.
Kugundua
mipango ya Simba SC kwenye eneo la kiungo na kuanza kutumia mipira
mirefu kushambulia no credit kwa GL ingawa Simba waliwatambua na muda
mwingi walikuwa wakipoteza mpira wanarudi nyuma haraka ( zonal marking )
Ni
dhahiri Yanga imekosa mtu wa mwisho kukaa na mpira , kushambulia na
kuwatengenezea wenzake . Licha ya Haruna Niyonzima kupangwa kama namba
10 lakini ilimpasa kutembea uwanja mzima kujaribu kuifumua midfield ya
Simba SC iliyokuwa ikiwazuia kupitisha mipira kati kitu ambacho
kiliondoa kombinesheni yake na Amisi Tambwe na kujikuta forward line
nzima ikikatika na kutegemea flanks kushambulia kupitia Kaseke , Msuva
au full backs Juma na Haji .
Mechi
imeamuliwa kwa matuta si mbaya ilistahili baada ya balance kimbinu na
kiufundi . Bado Yanga wana jinamizi la Penati . Wanahitaji kuliondoa kwa
mazoezi mengi .
Mchezaji
bora kwa ujumla katika mchezo huu ni Besala Bukungu beki namba mbili wa
Simba SC . Ameonesha ukomavu na faida ya ukongwe kuisadia Simba kwenye
marking na kushambulia.
Asanteni
0 comments :
Post a Comment