.
1.idadi yote ya
wabunge wa viti maalumu katika bunge ni asilimia 40 ya viti vyote vya
bunge katika majimbo yote(40% of all seats/constituencies ).
idadi ya viti vya ubunge ama majimbo kwa sasa ni 264.
40% ya 264 ni ngapi? unaweza kupiga kujua kutakuwa na jumla ya viti maalum wangapi.
FURSA YA CHAMA KUPATA WABUNGE VITI MAALUMU.
kwanza ili chama husika kiweze kupata wabunge wa viti maalumu ni sharti
chama hicho kiwe na jumla ya kura zisizopungua asilimia 5 ya kura zote
za wagombea wote wa ubunge wa chama hicho katika jumla ya kura zote za
wabunge wa vyama vyote.
Hii bila kujalisha kama chama kimeshinda
wabunge ama hakikushinda katika majimbo kiliyogombea. Hata kama chama
kimeshindwa katika majimbo yote lakini kikafanikiwa kupata kura
zinazofikia asilimia 5 ya kura zote za wabunge wa vyama vyote basi chama
hicho kinapata fursa ya kuwa na wabunge wa viti maalumu.
kwa hiyo ieleweke wazi kuwa idadi ya wabunge walioshinda haitumiki kupata wabunge viti maalumu.
mbunge aliyeshinda kutoka jimbo la wapiga kura wachache mathalani
majimbo ya Zanzibar atakuwa na kura chache pengine kuliko mtu
aliyeshindwa katika jimbo la wapiga kura wengi kama majimbo ya mjini Dar
es salaam.Hivyo huyu aliyeshindwa anaweza kuchangia zaidi kupatikana
kwa mbunge wa viti maalumu kuliko aliyeshinda kwa mfano huu niliotoa.
na kwa vyovyote vile majimbo ya Zanzibar yanachangia asilimia ndogo
sana katika viti maalumu. Mchango wa kura za viti maalumu katika majimbo
yote ya Zanzibar yenye jumla ya wapiga kura laki 4 na ushehe ni mdogo
kuliko mchango wa majimbo yote ya mkoa wa Shinyanga ulio na wapiga kura
wapatao laki 7.
kwa hiyo hapa ni mchezo wa kupata kura nyingi zaidi na si kushinda viti vingi zaidi vya ubunge.
MGAWANYO WA HAO WABUNGE.
ili kupata kila chama kinapaswa kugawiwa wabunge wangapi inabidi
asilimia ya kura za wabunge wote waliogombea katika kila chama dhidi ya
kura zote za vyama vinavyostahili kupata wabunge viti maalumu
ikokotolewe na hiyo itasaidi kujua kila chama kitapata asilimia ngapi
kati ya hao wabunge wote(40% of 264). Idadi hiyo ipe jina la M.
kuna mazingira ambayo chama hakikusimamisha wagombea ubunge ama mgombea
ubunge wake alipita bila kupingwa katika jimbo. Katika mazingira haya
hakuna kura halali za mbunge kwa chama husika zilizopigwa na wapiga
kura.
kwa hiyo ili kupata idadi ya kura zote zingatia mambo yafutayo.
1.Jumla ya kura zote za wagombea ubunge wa chama hicho katika maeneo
kilichosimamisha wagombea ni sehemu ya kura zinazotumika. ziite jina la
kura X.
2.Jumla ya kura zote za mgombea urais katika maeneo
ambayo chama hicho hakikusimamisha mgombea ubunge zitahesabiwa kuwa ni
kura za ubunge za chama hicho, Ziite jina la kura Y.
Mfano katika
jimbo la Kinondoni ambapo Chadema haikusimamisha mgombea ubunge bali
alisimamishwa wa CUF (UKAWA) basi kura za Edward Lowassa(mgombea Urais)
katika Jimbo hili zitahesabiwa kama kura za mgombea ubunge wa chadema
kwa swala la viti maalumu katika jimbo hili la kinondoni.
na hizo
za mbunge wa CUF kinondoni zinaingia katika hesabu ya CUF. zile za
mgombea wa CCM alieshindwa bwana IDD AZAN zinaingia katika hesabu ya
CCM.
3.kama chama kimepita bila kupingwa katika jimbo. Maana yake
uchaguzi haukufanyika kabisa kwa kuwa mgombea alikuwa mmoja tu na hivyo
hakuna kura zilizopigwa. Kwa mazingira haya hapa kura za Rais
hazitahusika. Kinachofanyika ni kukokotoa asilimia 51 ya wapiga kura
wote walioandikishwa katika jimbo hilo bila kujali walijitokeza wote
kupiga kura ama laa. (51% of registered voters in that
constituency).Ziite jina la kura Z.
asilimia hizo zinahesabiwa
kuwa ni kura halali za mgombea huyo aliyepita bila kupingwa ambazo
zinapaswa kutumika wakati wa kukokotoa wabunge wa viti maalumu.
kwa kuwa mwaka huu hakuna mbunge aliyepita bila kupingwa basi kipengere
cha 1 na 2 ndivyo vitatumika kukokotoa idadi ya vitu maalumu kwa kila
chama.
hesabu ni kama hivi.
X + Y + Z= kura zote za ubunge za kila chama.
NB:
1.kama chama hakima mgombea urais Y= 0 kwenye mazingira ya Y.
2. kwa kuwa hakuna mbunge aliyepita bila kupingwa nchi nzima basi Z=0 kila mahali.
(a). Chadema=X+Y+Z= P1
(b). CUF=X+Y+Z=P2
(c). CCM=X+Y+Z=P3
kura zote walizopigiwa wabunge.
P1+P2+P3+P4+............+Pn=W (Jumla ya kura za wagombea ubunge wote
toka vyama vyote vilivyosimamisha wagombea). W itatumika tu kujiridhisha
kama chama kinastahili kupata wabunge viti maalumu na si vinginevyo.
hapa kuna kura za vyama ambavyo havitapata viti maalumu kama ACT, NRA,
CHAUMA nk nazo zinaingizwa katima jumla ya kura zote zilizopigwa kwa
wagombea wabunge wote.
lakini mgawanyo wa asilimia kwa vyama utahusisha tu vyama vyenye sifa ya kupata wabunge wa viti maalumu.
kwa hiyo chukua P1+P2+P3=Q. na utafute asilimia ya kila chama katika hivyo vitatu.
lakini sina uhakina kama CUF imefikisha asilimia 5 ya kura zote kwa
maana ya P2.kwa kuwa wagombea wengi wametoka Zanzibar kuliko na wapiga
kura wachache ama kura chache.(mpaka kujiridhisha kwa CUF).
(i). viti maalumu chadema.
(P1/Q x 100) x M= Viti maalumu chadema.
(ii). viti maalumu CUF.
( P2/Q x 100) x M=viti maalumu CUF.
(iii). viti maalumu CCM.
(P3/Q x 100) x M= viti maalumu CCM.
M ni jumla ya wabunge wote wa viti maalumu bungeni
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment