BOMOA BOMOA YAHAMIA KWA KASI DODOMA

 ZAIDI ya nyumba 140 mjini Dodoma zimebomolewa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kutokana na wananchi kujenga kiholela katika maeneo yasiyoruhusiwa huku Jeshi la Polisi likilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wakileta fujo ikiwemo kufunga barabara kuu ya Dodoma – Singida.Bomoabomoa hiyo imefanyika katika maeneo ya Chinangali, Ndachi, Barabara ya Bahi na Kizota Dampo katika eneo la Kizota licha ya kutolewa notisi ya siku saba kwa wananchi hao kuondoka, lakini walikaidi amri hiyo ndipo Jeshi la Polisi pamoja na watendaji wa CDA walianza kazi hiyo.
Hata hivyo, wananchi ambao hawakukubaliana na kazi hiyo, walianza kuwarushia polisi mawe.Baadhi ya wakazi waliangua vilio wengine wakipoteza fahamu baada ya kushuhudia nyumba zao zikibomolewa.Wakizungumza nje ya nyumba zao, baadhi ya wananchi walisema kazi hiyo ni ya ghafla na hawakupewa taarifa na hawaelewi hatma ya maisha yao kwani hawana pa kulala.
Mkazi wa Kizota Dampo, Mwajuma Khamis alisema alikuwa akitegemea nyumba hiyo kwa ajili ya makazi na sasa hana pa kwenda kufuatia bomoabomoa hiyo.

Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment