USHUHUDA;NILINYOLEWA NYWELE ZOTE SEHEMU ZA SIRI NA WACHAWI USIKU NIKIWA NIMELALA
Naitwa Prisca
mwenyeji wa mkoa wa Arusha napenda nishuhudie kitu ambacho kimetokea maishani
mwangu hadi kupelekea kuokoka. mwaka 2010 kwa sababu ya kutafuta maisha
nilikwenda zanzibar kuishi huko na nilipata chumba cha kupangwa maeneo ya
airport na niliishi vizuri tu na majirani ambao tulikua tumepanga pamoja na
kama binadamu ukiwa bado unayapenda ya dunia na shetani ametawala maisha yako
niliamua kuwa na mpenzi mwanajeshi na uhusiano wetu uliendelea kwa muda kidogo.
Baada kama ya miezi 6 nilianza kupatwa na matatizo mara niugue ghafla na
nikienda kupima naambiwa sina ugonjwa wowote na hadi nilienda kwa mganga wa
kienyeji maeneo ya unguja ukuu lakini ndio kwanza matatizo yaliongezeka. Baada
kama ya mwezi mmoja baadaye vituko viliongezeka maana siku moja nilikuta nywele
upande mmoja wa kichwa zimenyolewa zote ukweli nililia sana na kusema MUNGU
mbona haya yananipata mimi? siku mbili baadae nikiwa natoka kazini maana
nilikua hotelia nilikuta watu wananiongea mimi na nilijificha ili nisikie kile
wanasema niliwasikia wakisema ''HILI LI DADA NI LI KICHWA NGUMU SANA YAANI
LICHA YA KULITUMIA MAJINI YAKALILALA NA LICHA YA KULINYOA NYWELE KICHWANI BADO
TU HALITAKI KUMWACHIA HUYU MWANAUME AMBAYE AMETUKATAA SISI WENYEJI NA
KULIKUBALI HILI JINGA SASA HUYU MWANAUME ATA-SHARE MAPENZI NA MAJINI YETU HADI
ATAMCHUKIA '' nilishtuka sana na kuanza kulia na baada ya muda nilisikia mmoja
akisema ''LEO NDIO FINAL NA BAADA YA LEO ATAMWACHA TU HUYU MWANAUME''
nilishindwa kujizuia na kutokea na kuwambia mbona kunitesa hivyo je kosa langu
ni nini? walicheka sana na dada mmoja kati yao akaniambia kama najipenda
niachane na Sam ambaye ndiye mpenzi wangu na tulikua tumepanga kuoana kabisa
niliingia ndani na kuanza kulia na jioni hiyo Sam alikuja na kunikuta nalia
lakini nilimdanganya kuwa tumbo linauma ndio maana nalia na yeye kunisaidia na
baadaye alienda kazini jioni hiyohiyo. siku hiyo nilisema silali ili nione
kitakachoendelea na hata sijui nini kilitokea maana nilijikua nimeshalala na
niliamka asubuhi na kukuta sehemu zangu za siri zimechafuka na pia kubwa kuliko
yote na ambalo limesababisha kuandika haya ni kuwa nywele zote za sehemu yangu
ya siri zilikua zimenyolewa na wembe nililia na kujiuliza maswali mengi sana
yasiyo na majibu kwamba hivi inawezekana kweli mtu ukanyolewa nywele zote za
sehemu ile bila kujijua? . Asubuhi waliendelea kunicheka na kusema
walichobakiza ni kuniua. Nilikaa bila amani kwa zaidi ya wiki tangu siku hiyo
huku kila siku nikisikia vitisho usiku kila siku mara kelele,miabga ya ajabu
ajabu,na vitisho vingi mwisho nikakata tamaa ya kuishi na siku moja nikawaza
kama ni kufa ngoja nikafie kanisani japokuwa mimi nilikua mpagani. Kesho yake
baada ya siku hiyo nilienda kanisani la kilokole na kukuta vijana na watoto
kama 7 wakiimba kwaya niliwauliza mchungaji yuko wapi wakaniambia mchungaji wao
yuko safarini Dar nilichukia sana na mkubwa wa wale vijana akanikaribisha kukaa
na kusikiliza nyimbo nikamwambia nina shida na mchungaji na nataka aniombee
kwani nina matatizo makubwa na nakalibia kufa yule kijana alinitazama na
kuniuliza kwamba '' UNAAMINI KWAM,BA YESU KRISTO ANAWEZA KUKUPONYA?''
nilikubali akaniambia nipige magoti na wao wataniombea kiukweli nilikataa maana
nilijua labda mchungaji pekee ndio anaweza kuniombea na si waoa ambao wote
nawazidi umri hata kama yule kaka kiongozi ni kama namzidi miaka 3 naye ni
mwanajeshi. Kaka yule alinisihi sana na kuniambia sio mchungaji anayeponya bali
anayeponya ni MUNGU na wao watamwomba MUNGU na mimi nitapokea uponyaji.
Nilikataa na kusema nitakuja siku mchungaji akirudi lakini moyo unakataa na
kusema naweza kufa kabla mchungaji kuja mikakubali lakini kwa masharti kwamba
aniwekee mkono yule kiongozi wao tu na sio wale watoto yule kaka akaniambia ni
mwamini MUNGU wanayemwabudu kwani hakuna linaloshindikana kwa JEHOVAH na
akaniambia kwamba nitashuhudia kanisani kile ambacho MUNGU atatenda kupitia
watoto hao kweli nilikubali kuombewa na wakaniombea nikapoteza fahamu na baada
ya muda nikazinduka nikiwa nimepona yule kijana akaniambia kwamba nilikua na
mapepo mengi sana lakini YESU amenifungua na kweli nilijihisi mwepesi na niko
tofauti sana na nilivyokuja na wakaniwekea mikono tena kuniombea ulinzi wa
MUNGU na baada ya hapo wakaniambia sitachezewa tena na wachawi labda tu
nimwache huyu YESU aliyeniponya . Niliwaahidi kwamba sitamwacha YESU na nitamshawishi
mchumba wangu naye aokoke. Nilirudi nyumbani hakuna aliyeniongelesha na yule
dada nilimkuta analia na kusema nimemkomesha kwani majini yake yote 51
yamekufa. sikusema kitu na nikaingia ndani na kumshukuru sana MUNGU hata kama
nilikua sijajua kuomba lakini kwa maneno machache niliomba. Tangu muda huo
sikupatwa na tatizo lolote na niliishi kwa furaha na niliamua kumweleza yote
mchumba wangu akashangaa na akakubali kuokoka hivyo tangu feb 2011 akaokoka na
baadae tukaoana na hadi sasa tuko ndani ya YESU. sina la kusema ila namshukuru
sana BWANA YESU kwa kuniponya na kuniokoa na hadi sasa niko salala sifa na
utukufu ni kwa MUNGU BABA wa mbinguni. AMEN. picha hii haihusiani na Prisca
lakini inaonyesha jinsi BWANA YESU anavyotenda miujiza kwa kuponya mangoja na
nkufungua kila kifungo cha adui kilichokuwa kimefunga watu
0 comments :
Post a Comment