Jana Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma Kusini ilofunguliwa na David Kafulila dhidi ya washtakiwa; Husna Mwilima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya uvinza kama msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa Serikali ilipokea pingamizi toka
Katika utetezi wa mawakili wa Kafulila Daniel Lumenyera na Tundu Lissu
waliomba mahakama itupilie mbali pingamizi hilo la wakili maarufu
Fungamtama kwa hoja kuwa ni usumbufu kwa mteja wao na halina mana yoyote
kwa kesi ya Msingi.
Leo Jaji anaesikiliza kesi hiyo Bi Leila amezingatia ombi la Fungamtama na utetezi Lumenyela na kuamua kutupilia mbali pingamizi hilo la wakili wa Husna na kumtaka Husna Mwilima kumlipa Kafulila gharama za usumbufu kwa kuweka mapingamizi yenye sura ya kupoteza muda na usumbufu.
leo Mahakama imendelea na hoja ya kutathimini gharama ya dhamana ambayo Mhe Kafulila atapaswa kuweka kama dhamana ya kesi ili kesi ya msingi iweze kuanza.
Uamuzi kuhusu kiasi gani Mhe Kafulila atalipa kama dhamana utatolewa kesho na Mahakama.

0 comments :
Post a Comment