Kutokana
na kufanikiwa kuwasajili Brian Majwega, Paul Kiongera na Danny Lyanga,
straika Hamis Kiiza wa Simba amesema kikosi chao
kimebadilika na sasa
kina mwonekano mpya wa ushindi.
Majwega
ni kiungo mshambuliaji kama ilivyo kwa Kiongera wakati Lyanga ni
straika, wengine waliosajiliwa na Simba wakati huu ni beki Novatus
Lufunga wa African Sports na straika Hija Ugando.
Kiiza
raia wa Uganda aliyewahi kuichezea Yanga, amejigamba kuwa ujio wa
wachezaji hao utaiongezea nguvu Simba na anaamini pia utamuongezea kasi
ya ufungaji.
Hadi
sasa Kiiza amefunga mabao nane sawa na Donald Ngoma wa Yanga wakati
straika wa Stand United, Elias Maguri akiongoza kwa kufunga mabao tisa
katika mechi 11.
Alisema
Simba sasa inakuja kivingine kwani usajili uliofanywa umezingatia
mahitaji ya timu na mashabiki wategemee mambo mazuri kutoka kwao.
0 comments :
Post a Comment