Moshi. Madiwani wawili wa chama cha demakrasia na maendeleo (Chadema), wanahojiwa na Polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma zinazoangukia katika makosa ya jinai.
Mmoja wa Madiwani hao kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, anahojiwa kwa tuhuma za kutishia kumuua kwa maneno, mbunge wa Jimbo hilo Joseph Selasini.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro,Flugence Ngonyani,jana alilithibitishia gazeti la mwananchi kukamatwa kwa madiwani hao kwa nyakati tofauti na kuhojiwa kisha kuachiwa kwa dhamana
Ngonyani alisema Diwani wa kata moja ya wilaya ya Rombo(Jina linahifadhiwa)  alifunguliwa shauri na mbunge Selasini, kwa kile alichodai kuwa alimtishia kumuua kwa maneno.
Kamanda Ngonyani alisema Mbunge huyo aliandika maelezo ya kuwa Diwani huyo alitishia kumuua na kwamba upelelezi juu ya tuhuma hizo umeanza.
Pia Diwani mwingine katika Manispaa ya Moshi,nae alishtakiwa kwa kosa la kumsambulia mkazi wa kata take na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili.
Kamanda alisema kuwa uchunguzi unaendelea ili kuweza kubaini kiini halisi cha ugomvi na kwamba watafikishwa mahakama upelelezi utakapo kamilika.

Hata hivyo kamanda Ngonyani hakufafanua ni lini matukio hayo yalitokea zaidi ya kusema Diwani wa Rombo alikamatwa mwishoni mwa wiki na yule wa Moshi mjini alikamatwa jana.
- See more at: http://kusini-tz.blogspot.com/2015/12/madiwani-chadema-mbaroni-kwa-kosa-la.html#sthash.oLVGYUVk.dpuf
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment