MBUNGE WA MAFINGA MH COSATO CHUMI ATEKELEZA AHADI YAKE KWA HOSPITALI YA WILAYA

Pichani Mbunge wa jimbo la Mafinga mji ni Cotato chumi akimkabidhi msaada wa  vitanda ,magodoro pamoja na vifaa mbalimbali  kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga dk Abdul Msuya juzi 
 baadhi ya waandishi wa habari wakifuatiliwa ugawaji wa vifaa hivyo wakati wa makabidhiano
 Mbunge wa Mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi vifaa hivyo kwa vitendo
Baadhi ya wadau na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM walihudhulia tukio hilo 

TATIZO la upungufu wa vitanda katika wodi ya akina mama na watoto katika hospitali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ambalo kwa muda mrefu limekuwa chanzo cha msongamano na uwalazimu baadhi ya wagonjwa kulala sakafuni sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya uongozi wa hospitali hiyo kupokea msaada wa vitanda na vifaa tiba kutoka kwa mdau wa maendeleo katika sekta ya afya.

mbunge wa Mafinga Mjini (CCM) Cosato Chumi alisema kuwa kwa muda mrefu hospitali hiyo ilikuwa ina upungufu wa vifaa mbalimbali ikiwemo vitanda hali iliyofanya kuandika maandiko mbalimbali kwa wahisani  wa nje ya nchi ili kuweza kumsaidia kupata vifaa hivyo .
  
Alisema kuwa umefika wakati sasa wadau mbalimbali, mifuko ya kijamii na makampuni kujenga utamaduni wa kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wagonjwa hospitalini kwani kufanya hivyo ni sehemu ya kurudisha kile wanachokitapa kwa jamii.

“Unajua afya ni kila kitu katika maisha ya binadamu hivyo lazima nitekeleze ahadi zangu nilizotoa wakati wa kampeni na wanachi lazima tufanye kazi kwa kujituma ili tumuunge mkono rais wetu ambaye anania ya ya kutuletea maendeleo na kuwataka wadau mbalimbali kusaidia jamii zenye mahitaji na kuacha kutegemea serikali pekee “ alisema
Chumi aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kuunga mkono kwa kufanya kazi kwa nguvu zote ili walete maendeleo kwa pamoja maana akifanya kazi pekee yake bila wao hawezi kuleta maendeleo pekee yake.
  
Msaada huo wa vitanda 16 na magodoro 11 na vitu mbalimbali umetolewa na taasisi binafsi inayojishughulisha na masuala ya afya ya nchini Astralia ijulikanayo kama “Rafiki Surgical Mission” kwa uratibu wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Mafinga mjini 

Alisema kuwa msaada huo aliopatiwa  na rafiki zao hawajatoa hata senti tano bali huwa marafiki hao wanachangishana fedha na kununua vifaa hivyo na kisha kuvisafirisha mpaka bandari kavu ambapo hapo ndio hutumia garama kusafirisha vifaa hivyo mpaka sehemu husika

“Ndugu zangu nadhani kila mmoja alikuwa akifahamu machungu waliyokuwa wakipata mama zetu wanapokuja kujifungua kwa kukosa sehemu za kujifungulia lakini leo hii msaada huu utatusaidia sana na yoyote
atakayeguswa na anaweza kuja na kuchangia chochote maana mufindi ni yetu sote na mufindi itajegwa na wanamufindi wenyewe”alisema

Alisema jambo kubwa lilokuwa likimuumiza kicha kila kukicha ni tatizo la vifaa katika hospital, elimu  pamoja na tatizo la maji hivyo ni wakati wawanamafinga kushikana kwa pamoja katika kusumkuma mbele gurudumu la maendeleo ili kuendana na kauli mbiu ya sasa ya HAPA NI KAZI TU.

Akipokea msaada huo kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mafinga dk Abdul Msuya alisema kuwa msaada wa vitanda hivyo na magodoro na  vifaa mbalimbali utakuwa umemaliza kabisa tatizo la vitanda hospitalini hapo licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kumalizika endapo kutatokea mdau mwingine kuwasaidi Kwa upande wake katibu wa ccm wilaya ya Mufindi Jimsoni Muhagama
alimpongeza mbunge huyo kwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo huku akimwambia kuwa ni wakati wa kutekeleza kazi kwa vitendo na wala si maneno kwani wananchi wanapaswa kutatuliwa kero mbalimbali zinazowakabili badala ya kupiga porojo zisizo na msingi .

Mhagama alisema kuwa kila mmoja anapaswa kuwajibika ipasavyo katika nafasi yake kwani kasi anayokwenda nayo Rais John Magufuli si ya mchezo bali ni ya mchaka mchaka na ili nchi iweze kusimama katika mstari ulionyoka kila mmoja anapaswa kucheza wimbo wa mchaka mchaka

‘’Huuu si wakati lelemama huu sio wakati mchezo mchezo ni wakati wa uwajibikaji ,hakika Tanzania tumepata kiongozi mchapa kazi tazama sasa ni siku ya 27 nchi inaongozwa na watu wanne lakini kila sektaa imenyoka na mimi  nasemaa Magufuli wanyooshe tu kwa kuwa watu walikuwa wakifanya kazi kwa mazoeya bila ya kuangalia madhara wanayopata
watanzania swengi

Hata hivyo Mhgama alisema kuwa kwa kuwa kipindi cha muda mchache nchi inaongozwa na watu wachache na nchi imesimama haoni sababu ya kuwa na baraza kubwa la mawaziri bali Rais Magufuli achague baraza dogo kama
la watu 10 ili kupunguza mzigo kwa serekali yake ya kuwa na mawziri wengi wasiokuwa na tija  .
UFAFANUZI WA TAARIFA KUWA TANESCO HAINUNUI NGUZO NCHINI BALI INAAGIZA AFRIKA KUSINI
Kwa takribani wiki moja sasa kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari na mijadala kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuwa TANESCO haitumii nguzo za umeme zinazozalishwa hapa nchini bali inaagiza nguzo hizo kutoka nchini Afrika Kusini.
Taarifa hizo zilidai kuwa Shirika lipo kwenye mchakato wa kutangaza zabuni ya nguzo 700,000 kwa gharama ya Dola za Marekani 115 milioni sawa na Sh 250 bilioni kwa mwaka 2015-2018 na kwamba sehemu kubwa ya pesa hizo zitatumiwa na kampuni za nje.
Habari hizo ziliendelea kusema kuwa uagizwaji huo wa nguzo unaenda kinyume na Sera ya serikali ya maendeleo ya kiuchumi inayohamasisha matumizi ya bidhaa za ndani. Kwanza tunakanusha kuwa taarifa hizo SI SAHIHI HATA KIDOGO, NI UZUSHI NA MAJUNGU yenye nia ovu na hatujui anayezisambaza ana nia gani. Tunapenda kufafanua kwamba TANESCO hufanya manunuzi yake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa. Shirika linapotaka kufanya manunuzi yoyote, linafuata kikamilifu Sheria ya Manunuzi Namba 7 ya mwaka 2011 pamoja na Kanuni zake (GN 446) ya mwaka 2013
Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi, Zabuni yoyote isiyozidi Sh bilioni 1 inatakiwa itangazwe Kitaifa na hakuna kampuni ya nje inayoruhusiwa kuomba zabuni hiyo. Zabuni yoyote inayozidi Sh bilioni 1 inatakiwa itangazwe Kimataifa ili Makampuni ya ndani na ya nje nayo yaombe na kushindanishwa. Kwa kuwa zabuni nyingi za nguzo zinazidi Shs bilioni 1 ndio maana TANESCO hutangaza zabuni hizo Kimataifa.
Aidha ili kuweka uwazi, Sheria hiyo ya Manunuzi inalitaka Shirika kutangaza kwenye magazeti kila mwanzo wa mwaka Mpango wake wa Manunuzi wa mwaka mzima (Annual Procurement Plan) na miaka yote TANESCO imekuwa ikitekeleza kifungu hicho.
Ukweli ni kwamba; kwa mwaka 2013 hadi 2015 kupitia Zabuni namba PA/001/12/HQ/G/148 TANESCO ilitangaza zabuni ya kuhitaji nguzo 133,800. Kati ya nguzo hizo Makapuni ya ndani yanayozalisha nguzo hapa nchini (Local suppliers) yalishinda Zabuni ya kusambaza nguzo 49,510, Makampuni ya Ndani ambayo yalishinda Zabuni na kuagiza nguzo hizo nje ya nchi yalikuwa na Zabuni ya nguzo 75,670 wakati Makampuni ya nje yalishinda Zabuni ya kusambaza nguzo 8,620 tu.
Kwa Zabuni ya mwaka 2014 hadi 2016 ambayo ilikuwa ni ya kuongezea mahitaji ya nguzo kutokana na kasi ya usambazaji umeme nchini, TANESCO kupitia Zabuni namba PA/001/14/HQ/G/113 ilitangaza Zabuni ya hitaji la nguzo 16,500. Katika zabuni hiyo Makapuni ya ndani yanayozalisha nguzo hapa nchini yalipata Zabuni ya kusambaza nguzo 1,600 wakati Makampuni mengine ya ndani lakini yanayoagiza nguzo hizo kutoka nje yalipata zabuni ya kuleta nguzo 14,900. Zabuni hii haikuwa na kampuni ya nje hata moja.
Zabuni Mpya ambayo habari hizo zilipotosha kuwa ni ya nguzo 700,000 si kweli. Zabuni hiyo Mpya ni Namba PA/001/2015/HQ/G/001 ya mwaka 2016 hadi 2018 ambayo imeshatangazwa kwa mahitaji ya nguzo 240,060 na bado wasambazaji hawajapatikana.
Makampuni ya ndani yanayosambaza nguzo TANESCO ni M/s Sao Hill Industries Ltd, M/s Farm Equipment (T) Ltd, M/s Mufindi Wood Poles Ltd, M/s Critical Engineering na M/s New Forests Treated Timber. Makampuni ya nje ni Rousant International Ltd, Treated Timber Product Ltd, Low’s Creek Treated Timber Ltd, Maqhilika Treated Timber Ltd na Vuka Timbers Ltd.
Hivyo TANESCO inawahakikishia wananchi kwamba, Shirika haliagizi nguzo zote nje kama ilivyoelezwa, bali kwa mujibu wa Sheria, nguzo hizo husambazwa na makampuni ya ndani na nje yanayopatikana kwa njia za Zabuni za ushindani.
Baadhi ya makampuni ya ndani yanaweza kuwa hayapati zabuni hizi kwa sababu za ubora hafifu na bei kuwa juu zaidi ikilinganishwa na za nje. Hata hivyo inachokitaka TANESCO ni unafuu kwa wateja wake.
Imetolewa na:
OFISI YA UHUSIANO 
TANESCO MAKAO MAKUU.
- See more at: http://mtanzaniatz.blogspot.com/2015/12/taarifa-kutoka-tanesco-kuhusu-kununua.html#sthash.ECcITfLZ.dpuf

Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment