POINT ZA MSINGI ALIZOWAAMBIA MAGUFULI WAFANYABIASHARA
1. Yeye anaipenda sana private sector, Serikali yake itatoa ushirikiano mkubwa ili ifanikiwe zaidi kwani Serikali inaihitaji lakini pia sekta binafsi inaihitaji Serikali.
2. Ninawaomba sekta binafsi muwe wazalendo kwa kufanya Biashara kwa uadilifu. Ya Kaisari mpeni kwa kasi ya Hapa Kazi tu!
3. Wakati wa Kampeni niliwakwepa wafanyabiashara makusudi ili wasinipe pesa zao ili tuje tufanye Kazi "Hapa Kazi Tu". Kama kuna mfanyabiashara aliyenipa hata shilingi mbili, ainue mkono.... hakuna!
4. Wafanyabiashara wa ndani mjiamini, Serikali itawaunga mkono. Fanyeni miradi yoyote, hata atakayetaka kuwekeza kwenye gesi awekeze. Hakuna nchi yoyote duniani ambayo imefanikiwa kujenga uchumi imara bila kuwajengea uwezo watu wake wa ndani! Tutawawezesha.
5. Wale waliokwepa ushuru wa makontena ninatoa Grace Period, ninawapa siku 7 wakalipe ushuru wetu, ndicho tunachohitaji na wakifanya hivyo tutawasamehe. Hawawezi kuendelea kukimbia kimbia na makontena, kwani siyo sindano. Baada ya siku Saba wajue hii ni Serikali inayoongozwa na John Pombe Magufuli.
6. Wenye uwezo acheni kunyanyasa wananchi. Huwezi kuhodhi eneo ambalo wananchi wengi wanalitumia kujiburudisha, ukawazuia kwenda hapo kwa sababu ya uwezo wako na ukazitumia Mahakama zetu.
0 comments :
Post a Comment