Kuanzia wiki ijayo, wiki ya mwisho ya Kampeni, tutakuwa na kampeni ya aina yake kuhakikisha tunamfikia kila mkaazi wa Arusha kukumbushana wajibu wetu wa kupiga kura kumchagua Mbunge wa Arusha Mjini, zoezi litakalofanyika Disemba 13, 2015.
Lengo letu ni kuhakikisha tunajitokeza wapiga kura wote zaidi ya laki 3 walioandikishwa Arusha Mjini na kupiga kura ili kuweka historia ya maamuzi ya kimsingi katika Jimbo letu.
Chadema tuna madiwani 33 kwenye Halamashauri yetu na wenzetu wana
Diwani mmoja tu. Tuna deni kubwa kuonesha tofauti ya Uongozi wenye tija
na Mabadiliko makubwa tuliyoyaahidi.
Mbunge Lema ni sehemu muhimu katika mafanikio haya ambayo tumeyapambania tangu 2010 mfululizo kwa shida, mateso na tabu nyingi.
Kwa wiki hiyo tutakuwa na ugeni wa viongozi wa kitaifa na baadhi ya wabunge watakaosambaa kwa kila kata, kila mtaa, kila kitongoji.
Tutawasiliana na kukumbushana tarehe ya kupiga kura Disemba 13 kwa njia zote za mawasiliano kwa teknolojia za sasa.
Asanateni sana kwa kuendelea kuniamini.

0 comments :
Post a Comment