Kama wewe ni miongoni mwa watu wa rika moja na mimi… Utakumbuka kuwa: Katika somo la Sayansi tulijifunza kuwa Pluto ni sayari ya mwisho katika mfumo wetu wa Jua. Lakini baada ya muda si mrefu ukakoseshwa mtihani kwa kujibu Pluto ni Sayari.
Pengine uliambiwa kwanini Pluto si sayari tena, au pengine mpaka leo ulikuwa unadhani Pluto ni moja ya sayari katika Mfumo wetu wa Jua…
Karibu tuiangalie kwa Undani Historia ya Pluto kupewa cheo cha U-Sayari, na hatimaye kwa huzuni: Kuvuliwa Cheo hicho:
Of course, hata kabla ya kugunduliwa kwake, wana-Astronomia walikwishabashiri tangu awali kwamba kuna Sayari ya tisa katika mfumo wetu wa Jua. Na kwa vile walikuwa bado hawajaiona, waliipa jina ’Planet X’.
Siku moja Tombaugh alipokuwa akifanya Kazi aligundua picha moja ya eneo la Anga ilionyesha kitu cha Ukubwa fulani kikiwa kwenye mwendo kama wa Sayari…
Baada ya Uchunguzi zaidi na utafiti wa zaidi ya mwaka mmoja, Tombaugh hatimaye alitangaza kwamba ameigundua ’Planet X’.
Na kwasababu, yeye na timu yake ndio walifanya Ugunduzi, wakapewa heshima ya kuipa jina Sayari hiyo. Walikuwa na majina mengi, lakini wote wakakubali kuipa jina ’Pluto’. Jina ambalo kimsingi lilitokana na pendekezo la mtoto wa miaka 11 aliyekuwa akisoma shule Oxford, Uingereza.
Kwa Hiyo baada ya Ugunduzi huo ikawa rasmi kwamba kuna Sayari tisa (9) katika mfumo wetu wa Jua.
Pamoja na Ugunduzi huo, na Uhakiki kwamba Pluto ilikuwepo, wana-Astronomia bado hawakuwa na uhakika wa ukubwa wake.
Mwaka 1978, mwezi wa Pluto uitwao ’Charon’ uligunduliwa. Na kwa kujua Uzito wake, wana-Astronomia wakaweza kujua ukubwa wa Pluto; kwamba ilikuwa na kipenyo (diameter) cha kilomita 2,400.
Ukubwa ambao uliifanya Pluto kuwa Sayari ndogo kuliko zote, ikifuatiwa na Utaridi (Mercury) yenye kipenyo (diameter) cha kilomita 4,880.
0 comments :
Post a Comment