Wanaastronomia wameweka msako wa kutambua kwa kiasi kikubwa kiwezekanacho cha sayari nebulae! Sayari nebulae katika
lugha rahisi ni gesi na mavumbi yenye kutoa mwanga huko angani, na pia
hazina uhusiano wowote na sayari. Kwa kutumia chombo cha X-ray cha
Chandra kinachomilikiwa na NASA, wanaastronomia wanajaribu kufuatilia
mawingu yote haya yaliyopo ndani ya galaxi yetu. Picha hii inaonyesha
sayari nebulae mbili za mbali ambazo tayari wameweza kuzipata!
Mawingu haya
yanatuonyesha lika ambalo nyota zote zenye ukubwa wa kati hupitia,
mfano wa nyota hizo ni Jua. Ambapo ikifika wakati nyota imeunguza
nishati yake yote, hutanuka na kutengeneza nyota kubwa iitwayo red giant.
Nyota hiyo ina uwezo wa kutanuka mara mia moja zaidi ya ukubwa wake wa
awali! Katika ukubwa huo mpya nyota hupata shida kushikilia tabaka lake
la nje la maada, hivyo kufanya kiasi kikubwa cha maada hizo kupotea na
kuingia katika anga la mbali.
Ingawa kiini
chenye joto jingi huachwa na kuanza kuangamia chenyewe, ambapo maada
zote zilizomo kwenye kiini huishia kugandamizwa katika nyota ndogo na
nzito. Nyota hiyo mpya huitwa nyota iliyodumaa “dwarf star”. Nyota
iliyodumaa yenye rangi nyeupe na uzito wa maada sawa na ule wa Jua letu
inaweza kuwa na ukubwa kama wa Sayari ya Dunia!
Gesi na
mavumbi yaliyotawanywa na nyota hutengeneza sayari nebula ( nebula ni
jina linawakilisha nebulae moja). Na nebula imeizunguka nyota iliyodumaa
na kutengeneza rangi za kupendeza, aina hii ya mizunguko hutokea katika
maumbo na ukubwa wa aina mbali mbali kama unavyoweza kuona hapa,
ambapo katika moja ya picha mawingu mawili yanayofuatana yanazunguka
katika kila pande za nyota na kufanya itengeneze umbo la mabawa ya
kipepeo!
Dokezo: Karibu
kila nyota itakuja kuwa sayari nebulae, likiwemo jua letu.
Wanaastronomia wanafikiri kuwa kuna karibu 30,000 sayari nebulae ndani
ya galaxi yetu peke yake!
0 comments :
Post a Comment