Don't Miss
Loading...
MUNGU NI NIA NJEMA
  • Home
  • HABARI ZA
    • MICHEZO
    • SIASA
    • KIMATAIFA
  • VICHEKESHO
    • MTAANI
    • MICHEZONI
    • MITANDAONI
  • AJIRA
  • ELIMU
  • SIASA
  • HABARI
Home / Uncategories / VIGOGO WANNE WA TAKUKURU AKIWEMO EDWARD HOSEA WATIMULIWA NA MAGUFULI

VIGOGO WANNE WA TAKUKURU AKIWEMO EDWARD HOSEA WATIMULIWA NA MAGUFULI

KAKSIGABA 8:55 AM Edit
Malisa Godlisten's photo.
Rais John Pombe Magufuli amemfukuza kazi aliyekua Mkurugenzi mkuu wa Tume ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Ndugu Edward Hosea kwa kile kilichoelezwa kutoridhishwa na utendaji wa TAKUKURU chini ya Hosea.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu inasema Magufuli ametengua uteuzi wa Hosea kutokana na kuendelea kushamiri kwa vitendo vya Rushwa nchini bila TAKUKURU kuchukua hatua zinazoridhisha.
Kufuatia hatua hiyo Magufuli amemteua aliyekuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi Valentino Mlowola kukaimu Nafasi ya Hosea. Kabla ya uteuzi huo Kamishna Mlowola alikua Mkurugenzi Msaidizi wa TAKUKURU nafasi aliyoitumikia kwa siku 12 tu tangu ateuliwe December 5 mwaka huu.
Kabla ya December 5, Mlowola alikua mkuu wa Idara ya Intelijensia ya Jinai ya Jeshi la Polisi, nafasi aliyoitumikia kwa miezi saba tu tangu alipoteuliwa na Rais Kikwete kushika wadhifa huo May mwaka huu.
Kabla ya hapo Mlowola alikua Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza (RPC) tangu mwezi October mwaka jana (2014). Hii ni kusema kuwa ndani ya mwaka mmoja (October 2014 hadi December 2015) Mlowola amepanda vyeo vinne kutoka RPC Mwanza, Kamishna wa Intelijensia jeshi la Polisi, Naibu Mkurugenzi TAKUKURU na sasa Kaimu Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewafukuza kazi viongozi wanne waandamizi wa TAKUKURU kwa kosa la kutotii agizo la Rais na kuamua kusafiri nje ya nchi wakati Rais amezuia safari za nje.
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nictus; ambao wote walisafiri nje ya nchi bila kuomba kibali kwa Rais au Katibu Mkuu Kiongozi.
Taarifa ya Ikulu iliyosomwa na Ombeni Sefue inatoa onyo kwa watumishi wote wa umma kutii agizo la Rais la kutokusafiri nje ya nchi na kama kuna ulazima waombe kibali ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi au kwa Rais mwenyewe.!
Share on Facebook Share on Twitter Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

RELATED POSTS

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments ( Atom )

Follow Me

  • Popular Post
  • Video
  • Category

Popular Posts

  • NAMNA YA KUSHINDA DHAMBI ILIYOKUTESA MUDA MREFU
    NITAISHINDAJE DHAMBI INAYONITESA? Na Mtumishi Peter Mabula. Ni ujumbe alioniandikia ndugu mmoja ambaye alihitaji msaada wa kiroho. Ndugu ...
  • NGOMA YA ASILI YA KABILA LA WACHAGA HUKO KILIMANJARO
  • SAYARI NA SIFA ZAKE
    MFUMO WETU WA JUA UNAUNDWA NA SAYARI NANE ZENYE SIFA TOFAUTI TOFAUTI KAMA IFUATAVYO; Mercury (Zebaki) Hii ni sayari iliyo karibu zaidi na...
  • VUNJA MBAVU SWAHILI COMEDY
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2015
    matokeo ya darasa la saba 2015
  • WARAKA WA ELIMU BURE HUU HAPA

Video Of Day

Labels

  • AJIRA
  • ELIMU
  • HABARI
  • MICHEZO
  • SIASA
  • UCHUMI NA AJIRA
  • VICHEKESHO

Broadcast live streaming video on Ustream

TANGAZA NASI SASA

TANGAZA NASI SASA

Football results provided by whatsthescore.com

Popular Posts

  • NAMNA YA KUSHINDA DHAMBI ILIYOKUTESA MUDA MREFU
    NITAISHINDAJE DHAMBI INAYONITESA? Na Mtumishi Peter Mabula. Ni ujumbe alioniandikia ndugu mmoja ambaye alihitaji msaada wa kiroho. Ndugu ...
  • NGOMA YA ASILI YA KABILA LA WACHAGA HUKO KILIMANJARO

CATEGORIES

  • AJIRA
  • ELIMU
  • HABARI
  • MICHEZO
  • RANDOM POSTS
  • SIASA
  • Slider
  • UCHUMI NA AJIRA
  • VICHEKESHO

Total Pageviews

UJUMBE WANGU

TUMWELEKEE MUNGU KWA MANENO NA MATENDO YETU
Copyright © 2014 MUNGU NI NIA NJEMA / Theme By : PAULCHAZZY - designed By PAULCHAZZY
  • HOME
  • PAULCHAZZY
  • CONTACT
  • NEWS