WANAANGA WASEMA MAJI YALIYOPO KWENYE JUPITA ALITOKA KWENYE KIMONDO

Jupita (Sumbula) ni sayari kubwa ya gesi na pia ni sayari kubwa kuliko zote katika mfumo wetu wa Jua, ina uzito wa asilimia 70% ya uzito wa sayari zote zikijumuishwa. Wanasayansi walipooiita Sumbula kama ni sayari kubwa ya gesi, hawakuipa sifa ya uongo kwani kama ukishuka na parashuti katika uso wa Jupita, unaweza usiguse ardhi ngumu. Katika maelfu ya kilometa unaweza ukawa unakatiza katika tabaka la hewa zito lenye dhoruba, kabla ya kufikia katika uso wa kushangaza wa sayari hiyo wenye bahari (ocean of exotic fluid) ya kina cha kilometa 40,000!

Herschel_Jupiter_WaterLakini maji haya ya ajabu ambayo mara nyingi yameundwa na haidrojeni sio bahari pekee iliyopo katika Sumbula. Picha hii inaonyesha ramani ya maji katika tabaka la hewa la sayari hiyo iliyotengenezwa na wanaastronomia! Ambapo waligundua kuwa karibu maji yote yaliletwa na chanzo cha kutoka nje, Kimondo cha Shoemaker-Levy 9 ambacho kiliigonga sayari hiyo mwaka 1994. Mgongano ambao ulikuwa wa kustaajabisha! Wakati kimondo hiki cha barafu kilipokuwa kinaingia katika tabaka zito la gesi na ukungu la Sumbula, kilitengeneza shimo kubwa jeusi, lenye kipenyo cha km 6,000 ambalo lilikuwa linaweza kuonyesha uso wa sayari katika picha na 2. Hiki hakikuwa kitu pekee kilichoachwa na kimondo cha Shoemaker-Levy; vimondo vingi hubeba kiasi kikubwa cha barafu katika viini vyake, na kwa hiki hakikuwa tofauti.
Kwa kutumia darubini ya angani ya Herschel, wanaastronomia wametengeneza ramani yenye pande tatu ya maji katika Sumbula, ambapo wingu la blue linaloizunguka sayari hiyo katika picha ni maji. Kuwepo kwa maji katika Sumbula sio jambo la kushangaza sana, lakini ramani inaonyesha kuwa maji mengi yanapatikana katika kizio cha kusini. Hii iliwashangaza wanaastronomia kwa sababu kama maji yalitoka ndani ya sayari basi walitegemea maji yatawanyike sawa katika pande zote. Kujirundika huku kwa maji katika sehemu moja kunaleta hitimisho moja tu: maji yaliletwa na kimondo cha Shoemaker-levy 9 tu!
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment