Nafahamu unajua kuwa Dunia si sayari pekee katika Mfumo wa Jua na kuwa kuna sayari nane kwa ujumla. Lakini sayari inayofanana na Dunia kwa kiasi kikubwa ni Mars, ambayo imepewa jina la utani ‘Sayari Nyekundu’ kutokana na uso wake kuwa na rangi nyekundu. Kwa sasa inazidi kudhihirika kuwa sayari hii ya Mars ilikuwa ya bluu kwa mda mrefu hapo mwanzo, ikiwa na maziwa, mito na bahari zinazotiririsha maji, kama ilivyo kwa Dunia!
Picha
hizi za kupendeza zilipigwa na chombo cha Mars Express, ambacho
kinaizunguka sayari ya Mars. Zinaonyesha mifereji ya mito ikikatiza
katika uso wa sayari, inaaminika kuwa mifereji hii ilitengenezwa na maji
yenye kina kirefu yaliyokuwa yanatiririka katika sayari hiyo katika
miaka mabilioni iliyopita kabla hata ya binadamu kuwepo!
Hata leo hii kuna maji katika sayari ya
Mars, ingawa yameganda chini ya uso wa sayari katika vizio vya Kaskazini
na Kusini (Kama Miamba ya Barafu iliyopo Duniani). Hivyo basi mifereji
hii ya mito inaweza isionekane kama ni kitu cha kushangazak, ingawa ni
mikubwa mno! Ikiwa na urefu wa kilometa 1,500, ambao ni urefu mkubwa
kupita hata mto Rhine ambao unakatiza bara la Ulaya kutokea Uholanzi
hadi Uswisi! Pia kina chake ni mita 300, ambacho ni kina kikubwa kupita
mto wowote upatikanao Duniani!
Picha hizi mpya kutoka katika chombo cha
Mars Express zinatupa mtazamo mpya wa historia ya sayari nyekundu na
kuifanya isionekane tofauti na dunia yetu ya leo!
Dokezo: Wanasayansi
wanaamini kuwa katika miaka mabilioni iliyopita sayari ya Mars
iliathirika na mafuriko makubwa, ambayo hayajawahi kutokea katika
historia ya mfumo wa Jua! Ni vigumu kutafakari kwa sasa, kwani siku hizi
sayari ya Mars ina baridi kali sana, na tabaka lake la hewa ni jembamba
sana kwa maji kuweza kutuama katika uso wake.
0 comments :
Post a Comment