YAYA TOURE AWANIA TUZO NYINGINE YA MCHEZAJI BORA WA AFRICA


Siku chache tu baada ya kutawazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika na shirika la BBC Yaya Toure, Image result for YAYA TOUREametajwa miongoni mwa wachezaji watatu bora kuwania taji la mwanakandanda bora mwaka huu na Shirikisho la soka barani Afrika (Caf).
Tuzo hii huwajumuisha wachezaji wa Afrika wanaocheza soka ng'ambo.
Nyota huyo wa Manchester City kwa mara nyengine atakuwa akipigania taji hilo dhidi ya mshambulizi wa Black Stars ya Ghana na Swansea Andre 'Dede' Ayew na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund.
Endapo atashinda kigogo huyo wa The Elephants ya Ivory Coast Yaya Toure, atakuwa mtu wa kwanza kunyakua taji hilo kwa mara ya tano.Image result for YAYA TOURE
Toure, ambaye aliiongoza Ivory Coast kutwaa ubingwa wa mataifa ya Afrika mapema mwaka huu pamoja na aliyekuwa nahodha wa Cameroon Samuel Eto'o ndio wachezaji wa pekee waliowahi kutwaa taji la mchezaji bora wa Afrika mara 4.
Eto'o alitwaa taji hilo katika miaka ya 2003, 2004, 2005 na 2010.
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment