MBUNGE WA JIMBO LA FUONI ZANZIBAR MHE. ABAAS MWINYI
Mbunge
wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe A bass Ali Hassan Mwinyi, akitembelea
Kituo cha Afya cha Fuoni Zanzibar kinachotowa huduma kwa Wananchi wa
Jimbo hilo na jirani wakati akitimiza ahadi yake kwa kutuo hicha,
akipata maelezo kutokwa kwa mdhamini wa kituo hicho Muuguzi wa Afya ya
Jamii Bi Mwaka Pandu Makame akitowa maelezo ya eneo lao la kuchomea taka
za kituo hicho.
Mbunge
wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassan Mwinyi akitembelea
kituo hicho cha Afya Fuoni Zanzibar akiwa katika ziara yake katika jimbo
lake kujiuonea ufanisi wa kituo hicho na kukabidha Madawa na kuvifanyia
mategenezo vyoo vya kituo hicho ni moja ya kero za Wananchi wanaofika
kituoni hapo.
Mbunge
wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Adass Mwinyi akitembezwa katika kituo
hicho na Madaktari wa Kituo hicho, akiwa katika ziara yake ya
kukamilisha ahadi yake juu ya kituo hicha kikifanyia mategenezo sehemu.
Mbunge
wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Mwinyi akimsikiliza daktari wa
kitengo cha kungolea meno katika Kituo hicho cha Fuoni Zainab Seif na
Khadija Khamis, wakimueleza Mbunge huyo baadhi ya vifaa vinakosekana
katika kitengo chao kwa ajili ya huduma ya kungolea meno Wananchi
wanaofika kituoni hapo. Kituo hicho kinatowa huduma za Uzalishaji wa
Kinamama kupiga Utra saund na huduma nyengine za matibabu
Mbunge
wa Fuoni Mhe Abass Mwinyi akizungumza wa Wafanyakazi wa Kitengo cha
Meno katika Kituo cha Afya Fuoni wakati wa ziara yake kutimia ahadi
alizotowa kwa Wananchi wa Jimbo hilo katika kituo hicho na kufanikisha
upatikanaji wa vifaa hivyo wanavohitaji katika kituo hicho kuondoa kero
kwa Wananchi wake wanaofika kituoni hapo kupata huduma ya meno na
nyeginezo.
Mhe
Abass Mwinyi akizungumza na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya Fuoni
Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa
kwa ajili ya kituo hicho, Kinachotowa huduma kwa Wananchi wa Jimbo lake
na Wananchi wa jirani.ili kuboresha ufanisi wa huduma ya Afya kituoni
hapo.
Mbunge
wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe. Abass Mwinyi akizungumza na wafanyakazi
wa Kituo hicho na Wananchi wa Jimbo lake wakati wa ziara yake ya kwanza
katika jimbo hilo na kukabidhi vifaa na Madawa kwa kituo hicho. Mhe
Mbunge Abass amesema sasa Hapa Kazi Tu, ili kuwaletea maendeleo Wananchi
wa Jimbo lake na kuondoa kero zote katika jimbo hilo na kuwa Jimbo la
mfano katika majimbo yote ya Zanzibar.
Daktari
Dhamana wa Kituo cha Afya Fuoni Said Fadhili Abass akizungumza wakati
wa mkutano huo na Mbunge wa Jimbo la fuoni na kumshukuru kwa msaada wake
huo kwa Kituo chao. na kusema dawa hizo zitatumika kwa wananchi wa
Jimbo hilo wanaofika kituoni hapa kupata huduma mbalimbali za Afya.
Wauguzi
wa Kituo cha Afya Fuoni wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Fuoni Mhe
Abass Mwinyi wakati akizungumza na Wafanyakazi hao katika ziara yake
kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa kwa ajili ya Wananchi
wanaofika kupata huduma kituoni hapo.Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi fedha shilingi milioni moja Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass, kwa ajili ya kutatua makero zinazokikabili kituo hicho cha Afya Fuoni ili kufanya kazi zao kwa kuwahudumia Wananchi kwa ufanisi zaidi.
Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi madawa Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass, kwa ajili ya matumizi ya kituo hicho kinachotowa huduma mbalimbali kwa Wananchi wa Fuoni zikiwemo za kuzalisha kinamama na upigaji wa vipimo vya utra sound katika kituo hicho na kulaza wagonjwa.
Mbunge
wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Ali Hassaan Mwinyi akimkabidhi
vifaa kwa akili ya vyoo vya kituo hicho Dakt. Dhamani wa Kituo cha Afya
Fuoni Zanzibar Said Fadhil Abass na kulia Muuguzi wa Afya ya Jamii
Kituoni hapo Mwaka Pandu Makame.
Mzee
wa Jimbo la Fuoni Mzee Takrima akizungumza wakati wa hafla hiyo ya
kukabidhi madawa na vifaa katika Kituo cha Afya Fuoni Zanzibar.
Wananchi wa Jimbo la Fuoni wakimsikiliza Mbunge wao.
Wauguzi
wa Kituo cha Afya Fuoni wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Fuoni Mhe
Abass Mwinyi wakati akizungumza na Wafanyakazi hao katika ziara yake
kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa kwa ajili ya Wananchi
wanaofika kupata huduma kituoni hapo.
Mwananchi
wa Jimbo la Fuoni akitowa shukrani na kumtaka Mbunge wa Jimbo hilo
kukabidhiwa gari ya wagonjwa kwa ajili ya kuihudumia kutowa huduma kwa
Wananchi wanaofika kituoni hapo kupata huduma gari hiyi hutumika kwa
Wananchi kesi zao zinapokuwa zimeshindikana hapo na kuhamishiwa katika
Hospitali ya Rafuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Sheha
wa Shehia ya Pangawe Jimbo la Fuoni akitowa shukrani kwa Mhe Mbunge
Abass Mwinyi kwa msaada wake katika Kituo chao na kumtaka Mbunge huyo
kufutalia ajira za Vijana wanaojitolea katika Kituo hicho sasa karibu
miaka miwili hufanya kazi ya kuwahudumia wagonjwa wanaofika kituo hapo
bila ya kuajiriwa amemuomba mbunge huyo kufuatilia swala hilo.
Wauguzi
wa Kituo cha Afya Fuoni na Wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la
Fuoni Mhe Abass Mwinyi wakati akizungumza na Wafanyakazi hao katika
ziara yake kutembelea Kituo hicho na kukabidhi madawa kwa ajili ya
Wananchi wanaofika kupata huduma kituoni hapo.
Mbunge
wa Jimbo la Fuoni Mhe Abass Mwinyi akiitikia dua baada ya kumalizika
kwa hafla hiyo ya kukabidhi vifaa katika kituo cha afya fuoni Zanzibar.
Wananchi na Waguzi wa kituo hicho wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kukabidhi vifaa.
Mbunge
wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Mwinyi akiwa na Wauguzi wa kituo
hicho wakibadilisha mawazo baada ya hfla hiyo akiwa katika eneo la kituo
hicho fuoni Zanzibar.
UFAFANUZI WA TAARIFA KUWA TANESCO HAINUNUI NGUZO NCHINI BALI INAAGIZA AFRIKA KUSINI
Kwa takribani wiki moja sasa kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya
habari na mijadala kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya
habari kuwa TANESCO haitumii nguzo za umeme zinazozalishwa hapa nchini
bali inaagiza nguzo hizo kutoka nchini Afrika Kusini.
Taarifa hizo zilidai kuwa Shirika lipo kwenye mchakato wa kutangaza
zabuni ya nguzo 700,000 kwa gharama ya Dola za Marekani 115 milioni sawa
na Sh 250 bilioni kwa mwaka 2015-2018 na kwamba sehemu kubwa ya pesa
hizo zitatumiwa na kampuni za nje.
Habari hizo ziliendelea kusema kuwa uagizwaji huo wa nguzo unaenda
kinyume na Sera ya serikali ya maendeleo ya kiuchumi inayohamasisha
matumizi ya bidhaa za ndani. Kwanza tunakanusha kuwa taarifa hizo SI
SAHIHI HATA KIDOGO, NI UZUSHI NA MAJUNGU yenye nia ovu na hatujui
anayezisambaza ana nia gani. Tunapenda kufafanua kwamba TANESCO hufanya
manunuzi yake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.
Shirika linapotaka kufanya manunuzi yoyote, linafuata kikamilifu Sheria
ya Manunuzi Namba 7 ya mwaka 2011 pamoja na Kanuni zake (GN 446) ya
mwaka 2013
Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi, Zabuni yoyote isiyozidi Sh bilioni 1
inatakiwa itangazwe Kitaifa na hakuna kampuni ya nje inayoruhusiwa
kuomba zabuni hiyo. Zabuni yoyote inayozidi Sh bilioni 1 inatakiwa
itangazwe Kimataifa ili Makampuni ya ndani na ya nje nayo yaombe na
kushindanishwa. Kwa kuwa zabuni nyingi za nguzo zinazidi Shs bilioni 1
ndio maana TANESCO hutangaza zabuni hizo Kimataifa.
Aidha ili kuweka uwazi, Sheria hiyo ya Manunuzi inalitaka Shirika
kutangaza kwenye magazeti kila mwanzo wa mwaka Mpango wake wa Manunuzi
wa mwaka mzima (Annual Procurement Plan) na miaka yote TANESCO imekuwa
ikitekeleza kifungu hicho.
Ukweli ni kwamba; kwa mwaka 2013 hadi 2015 kupitia Zabuni namba
PA/001/12/HQ/G/148 TANESCO ilitangaza zabuni ya kuhitaji nguzo 133,800.
Kati ya nguzo hizo Makapuni ya ndani yanayozalisha nguzo hapa nchini
(Local suppliers) yalishinda Zabuni ya kusambaza nguzo 49,510, Makampuni
ya Ndani ambayo yalishinda Zabuni na kuagiza nguzo hizo nje ya nchi
yalikuwa na Zabuni ya nguzo 75,670 wakati Makampuni ya nje yalishinda
Zabuni ya kusambaza nguzo 8,620 tu.
Kwa Zabuni ya mwaka 2014 hadi 2016 ambayo ilikuwa ni ya kuongezea
mahitaji ya nguzo kutokana na kasi ya usambazaji umeme nchini, TANESCO
kupitia Zabuni namba PA/001/14/HQ/G/113 ilitangaza Zabuni ya hitaji la
nguzo 16,500. Katika zabuni hiyo Makapuni ya ndani yanayozalisha nguzo
hapa nchini yalipata Zabuni ya kusambaza nguzo 1,600 wakati Makampuni
mengine ya ndani lakini yanayoagiza nguzo hizo kutoka nje yalipata
zabuni ya kuleta nguzo 14,900. Zabuni hii haikuwa na kampuni ya nje hata
moja.
Zabuni Mpya ambayo habari hizo zilipotosha kuwa ni ya nguzo 700,000 si
kweli. Zabuni hiyo Mpya ni Namba PA/001/2015/HQ/G/001 ya mwaka 2016 hadi
2018 ambayo imeshatangazwa kwa mahitaji ya nguzo 240,060 na bado
wasambazaji hawajapatikana.
Makampuni ya ndani yanayosambaza nguzo TANESCO ni M/s Sao Hill
Industries Ltd, M/s Farm Equipment (T) Ltd, M/s Mufindi Wood Poles Ltd,
M/s Critical Engineering na M/s New Forests Treated Timber. Makampuni ya
nje ni Rousant International Ltd, Treated Timber Product Ltd, Low’s
Creek Treated Timber Ltd, Maqhilika Treated Timber Ltd na Vuka Timbers
Ltd.
Hivyo TANESCO inawahakikishia wananchi kwamba, Shirika haliagizi nguzo
zote nje kama ilivyoelezwa, bali kwa mujibu wa Sheria, nguzo hizo
husambazwa na makampuni ya ndani na nje yanayopatikana kwa njia za
Zabuni za ushindani.
Baadhi ya makampuni ya ndani yanaweza kuwa hayapati zabuni hizi kwa
sababu za ubora hafifu na bei kuwa juu zaidi ikilinganishwa na za nje.
Hata hivyo inachokitaka TANESCO ni unafuu kwa wateja wake.
Imetolewa na:
OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU.
Desemba 04, 2015
- See more at: http://mtanzaniatz.blogspot.com/2015/12/taarifa-kutoka-tanesco-kuhusu-kununua.html#sthash.ntfbk93W.dpuf
0 comments :
Post a Comment