SIMBA; BRIAN MAJWEGA WETU RAUNDI BAADA DIRISHA DOGO KUFUNGWA

Taarifa kuhusu Brian Majwega
Ndugu wanachama na wapenzi wa Simba kama ambavyo tutakumbuka ni zaidi ya wiki mbili sasa tangu mchezaji Brian Majegwa akubaliwe kufanya mazoezi na kikosi cha Simba baada ya kupokea barua yake ya kuomba kufanya hivyo.
Ni jambo ambalo halifichiki kuwa mchezaji Majwega alionesha dhahiri kupenda kuendelea kuchezea kikosi cha Simba na hivyo ilitulazimu kwanza kumkabidhi kwa benchi la ufundi chini ya kocha wetu Dylan Kerr ili waweze kutupa tathimini kama wangependa Majwega kuendelea kubaki na kikosi cha Simba kikosi cha Simba.
Baada ya kupata ripoti kutoka katika benchi letu la ufundi kuwa kiwango cha Majwega kinaweza kusaidia kikosi cha Simba na kwakuwa mchezaji mwenyewe Majwega alionesha nia ya kutaka kuendelea kubaki na kikosi cha Simba hivyo uongozi wa Simba na uongozi wa Azam FC ulikutana kujadili suala hili na mpaka sasa mazungumzo yanaonesha kuwa kwa asilimia kubwa mchezaji Brian Majegwa atachezea klabu ya Simba baada ya kufungwa kwa dirisha dogo.
Ni imani yetu kuwa mazungumzo yatamalizika vizuri na mchezaji Majwega kuweza kwenda kwenye klabu ambayo anatamani kuichezea kwa sasa.
Imetolewa na
Haji S. Manara
Mkuu wa mawasiliano
SIMBA NGUVU MOJA
Share on Google Plus

About KAKSIGABA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment