Wingu la rangi ya chungwa katika picha
linaonyesha mabaki yanayotokana na nyota iliyotengenezwa katika kiini
chake. Aina hii ya mawingu huwa na aina zote za malighafi kwa ajili ya
kutengeneza Sayari! Lakini kama wanaastronomia wanataka kujua ni kiasi
gani cha sayari wingu hili linaweza kutengeneza, wanahitaji kujua uzito
wake kwanza.
Njia rahisi na yenye akili wanayoitumia
ni kuangalia nyota zilizo jirani ili kupata msaada, kwani visahani vya
mawingu vilivyo karibu vinaweza kuonekana vizuri na kutoa taarifa nyingi
kuliko vile vilivyo mbali. Baada ya kuvisoma visahani hivyo,
wanaastronomia wamefahamu kuwa kuna mpangilio unaofanana katika aina hii
ya visahani! Kwani kwa kila punje ya haidrojeni ya kawaida kuna kiwango
maalum cha gesi kiitwacho haidrojeni nzito.
Hii imekuwa ni bahati kubwa kwa
wanaastronomia, kwa sababu haidrojeni nzito ni rahisi kuitambua hata
katika umbali mrefu sana. Hii inamaanisha kuwa wanaweza kukokotoa kiasi
cha haidrojeni ya kawaida katika visahani vilivyo mbali. Kwa kuongeza
kiasi cha haidrojeni ya kawaida katika uzito wa maada nyingine katika
kisahani, wameweza kugundua kwa ufasaha uzito wa kisahani kizima.
Imegundulika kuwa kisahani kilichopo
katika picha kina maada za kutosha za kuweza kutengeneza sayari nane za
mfumo wetu wa Jua, na bado nyingine zikabaki! Kisahani cha wingu
kinachozunguka nyota hii kina maada za kutosha kuweza kutengeneza sayari
50 zenye ukubwa kama Jupita na kila moja kuwa na ukubwa wa kumeza
sayari kama Dunia mara 1000!
Dokezo: Katika uchunguzi
mwingine, wanasayansi wamegundua kuwa kisahani hiki hiki kina maji ya
kutosha kuweza kujaza bahari maelfu zilizopo Duniani!
0 comments :
Post a Comment